Korona imeiokoa Serikali (Mtazamo wangu)

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli kwa miaka minne imekuwa ikiwadanganya wafanyakazi juu ya kuwaongeza mishahara Yao.

Wakati wanapiga kampeni CCM na Rais Magufuli waliwaahidi wafanyakazi kwamba watawaongeza mishahara Yao lakini kila mwaka Rais Magufuliakialikwa kwenye sherehe za meimosi anaongea vitu ambavyo wafanyakazi wenyewe hawavielewi.

Leo ni Mei mosi Rais Magufuli anafunga miaka yake mitano ya kuwapiga sound wafanyakazi nadhani korona Leo itakuwa kisingizio kwasababu hatakutana nao uso kwa uso hivyo nyani (wafanyakazi) watauwawa bila huruma kwani hawatakuwa na eye contact na mkulu.

Poleni wafanyakazi ila pigeni mzigo malipo ni kwa Mungu baba.
 
Tumepatikana!
IMG_20200501_071909.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama hakuna maandamano, Tunaamini Mhe Rais anaweza kupitia vyombo vya Habari akawaambia Watanzania maneno mazuri ya ukweli kukidhi matarajio yao ya subira ya miaka 5 bila nyongeza ya mishahara na kupanda madaraja kwa walio wengi. Waliofanikiwa zaidi ni wale tu waliopata nafasi za madaraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyakazi huku MTAANI wanasema serikali imetupiga goli 5-0 ila wanasema poaaaaa

Sasa hi poaaaaa sijui inamaanisha Nini. Ha ha ha ha ha nimewacheka nhiiiiiiiiiiiii wafanyakazi
 
Corona inakwenda kuifagia serikali na kuacha kovu kubwa kwenye jamii. Kila mmoja ataguswa tu, watakaobaki labda watapata akili za kuchagua viongozi na sio watawala.
 
Wengi tulishafahamu kitambo hakuna kitakacho tokea. Ameanzisha mamiradi mengi makubwa na ambayo yanakomba tu hela zetu za ndani na kuzipeleka nje.

Baadhi ya watu wanafurahia sana wafanyakazi kuishi maisha magumu! Wamesahau ya kwamba karibia kiasi chote fedha za hao wafanyakazi wanazopata kama mishahara au hata mikopo, huziingiza tena mtaani kupitia manunuzi mbalimbali au kusaidia familia zao, nk. na hivyo kuendeleza mzunguko wa fedha kwa makundi mbalimbali.

Makosa ya kujenga mamiradi makubwa na kwa fujo, hata Nyerere aliyafanya enzi zake, na mwisho wa siku yalitugharimu kama Taifa. Unaweza ukawa na nia njema kabisa ya kufanya kitu, ila njia utakayoitumia ndiyo itakayo kutofautisha wewe na mwingine. JK alifanya yote kwa pamoja, ila mwenzangu na mimi yeye anawaza miundombinu tu.
 
Hilo lilitarajiwA... Wala hAkuna mtumishi ana habari nae. Afanye yake. Mungu yupo!
 
Aliekudanganya wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kakudanganya,sekta zote za.serikali wameongezwa mishahara kimyakimya,na wanalipwa kwa wakati ,na ndio maana wapo kimya ,lengo lilikuwa wafanyabiashara wanatabia serikali ikiongeza mishahara na wao hupandisha bei,lengo ni kudhibiti mfumuko wa bei,

Kwakua wewe ni jobless hii mada inakuzidi kimo
Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli kwa miaka minne imekuwa ikiwadanganya wafanyakazi juu ya kuwaongeza mishahara Yao.

Wakati wanapiga kampeni CCM na Rais Magufuli waliwaahidi wafanyakazi kwamba watawaongeza mishahara Yao lakini kila mwaka Rais Magufuliakialikwa kwenye sherehe za meimosi anaongea vitu ambavyo wafanyakazi wenyewe hawavielewi.

Leo ni Mei mosi Rais Magufuli anafunga miaka yake mitano ya kuwapiga sound wafanyakazi nadhani korona Leo itakuwa kisingizio kwasababu hatakutana nao uso kwa uso hivyo nyani (wafanyakazi) watauwawa bila huruma kwani hawatakuwa na eye contact na mkulu.

Poleni wafanyakazi ila pigeni mzigo malipo ni kwa Mungu baba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli kwa miaka minne imekuwa ikiwadanganya wafanyakazi juu ya kuwaongeza mishahara Yao.

Wakati wanapiga kampeni CCM na Rais Magufuli waliwaahidi wafanyakazi kwamba watawaongeza mishahara Yao lakini kila mwaka Rais Magufuliakialikwa kwenye sherehe za meimosi anaongea vitu ambavyo wafanyakazi wenyewe hawavielewi.

Leo ni Mei mosi Rais Magufuli anafunga miaka yake mitano ya kuwapiga sound wafanyakazi nadhani korona Leo itakuwa kisingizio kwasababu hatakutana nao uso kwa uso hivyo nyani (wafanyakazi) watauwawa bila huruma kwani hawatakuwa na eye contact na mkulu.

Poleni wafanyakazi ila pigeni mzigo malipo ni kwa Mungu baba.
Hio sounds ipo tu hata corona isingekuwapo, muhimu wafanyakazi wajiongeze tu October
 
Back
Top Bottom