Painkiller Malenga Sera
New Member
- Mar 30, 2020
- 4
- 0
Korona imetushinda,yatutia sononeko
Mazao tuliyopanda,bangi miraa tumbako
Kuuza tunapoenda,wateja hawapo soko
Eti ndiko kuzuia,Korona isizagae.
Magunia ya makaa,tulochoma msituni
Siku mbili yamekaa,stendi gari hatwoni
Serikali mekataa, gari kwingia mjini
Eti ndio kuzuia, Korona izisambae.
Ifikapo saa moja,kinywa chao kimenena
Nti nzima kila mja,si ndani ‘kipatikana
Ataiona miuja, tangu kale hajaona
Eti ndio kuzuia, Korona izipambae.
Tukutuku na matatu, zibebazo abiria
Zibebe wachache watu, si wengi kupindukia
Abiria wasifutu, barakao kuvalia
Eti ndio kuzuia, Korona izimomae.
Ukienda kila kona, mijini na mashambani
Vieuzi utaona, maji ndoo na beseni
Muaji tusomuona, tukimuosha jamani!
Eti ndiko kuzuia, Korona izienee.
Ifikapo saa moja,kinywa chao kimenena
Nti nzima kila mja, si ndani ‘kipatikana
Ataiona miuja, tangu kale hajaona
Eti ndio kuzuia, Korona izipambae.
Tukutuku na matatu,zibebazo abiria
Zibebe wachache watu, si wengi kupindukia
Abiria wasifutu, barakao kuvalia
Eti ndio kuzuia, Korona izimomae.
Ukienda kila kona, mijini na mashambani
Vieuzi utaona, maji ndoo na beseni
Muaji tusomuona, tukimuosha jamani!
Eti ndio kuzuia, Korona izienee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mazao tuliyopanda,bangi miraa tumbako
Kuuza tunapoenda,wateja hawapo soko
Eti ndiko kuzuia,Korona isizagae.
Magunia ya makaa,tulochoma msituni
Siku mbili yamekaa,stendi gari hatwoni
Serikali mekataa, gari kwingia mjini
Eti ndio kuzuia, Korona izisambae.
Ifikapo saa moja,kinywa chao kimenena
Nti nzima kila mja,si ndani ‘kipatikana
Ataiona miuja, tangu kale hajaona
Eti ndio kuzuia, Korona izipambae.
Tukutuku na matatu, zibebazo abiria
Zibebe wachache watu, si wengi kupindukia
Abiria wasifutu, barakao kuvalia
Eti ndio kuzuia, Korona izimomae.
Ukienda kila kona, mijini na mashambani
Vieuzi utaona, maji ndoo na beseni
Muaji tusomuona, tukimuosha jamani!
Eti ndiko kuzuia, Korona izienee.
Ifikapo saa moja,kinywa chao kimenena
Nti nzima kila mja, si ndani ‘kipatikana
Ataiona miuja, tangu kale hajaona
Eti ndio kuzuia, Korona izipambae.
Tukutuku na matatu,zibebazo abiria
Zibebe wachache watu, si wengi kupindukia
Abiria wasifutu, barakao kuvalia
Eti ndio kuzuia, Korona izimomae.
Ukienda kila kona, mijini na mashambani
Vieuzi utaona, maji ndoo na beseni
Muaji tusomuona, tukimuosha jamani!
Eti ndio kuzuia, Korona izienee.
Sent using Jamii Forums mobile app