Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Haya ndio majibu ya waliokusikiliza Kiongozi mkuu.
Screenshot_2020-05-22-06-20-23.png
 
Serikali inajifanya masikini jeuri kumbe chini kwa chini inawalamba miguu mabeberu, inaomba samahani, inaomba radhi.

Chini kwa chini inabembeleza isamehewe ila huku nje sisi matajiri, sisi nchi huru hatupangiwi, sisi donor country, 😂😂😂.

Tumesema sana hii mikopo mnayochukua kutoka kwenye taasisi za kibiashara ni ghali sana, utasikia deni ni himilivu, nchi bado inakopesheka kumbe mnaficha madeni wa wafadhili wenu, sasa yamewafika kooni mmeenda kuwalamba makalio.

Uongozi ni akili.
 
Huu ugonjwa utaua watanzania wengi na mbaya zaidi itakuwa mwendo wa kimya kimya! Nina uhakika aliyezembea wakwanza ambaye mnamuabudu atakufa kwa huu ugonjwa

Mbona yale matakwimu ya vifo kwa kigogo hayapo tena kulikoni?
 
Hao watu 3% wamekufa wapi? Watu wote wa mkoa wa Njombe wafe afu hali iwe kama ilivyo, Subutuuu.

Kwa hili, nampongeza Raisi, he was a visionary.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani amekuambia Corona imekwisha duniani? Ugonjwa huu hauna mipaka na haupokei amri toka kwa mtu yoyote, kumbuka Waziri Mkuu wa Uingereza aliugua na maana wa mfalme wa Uingereza naye aliugua.
MAISHA YAKO YAKO MIKONONI MWAKO.
 
Ahsante Zitto kwa hizo taarifa chache ulizozitoa "descriptively". Kuna haja pia ya kuzifanyia kazi hizi takwimu zaidi ya hivi ulivyoweka "descriptively" ili kuweza kuwa na hoja dhahiri ya matokea ya corona katika uchumi wa nchi. Bahati mbaya hii si kazi yako wewe kama mwanasiasa. Sijui wana zuoni wetu wamepotelea wapi! Dunia nzima kwa sasa, sekta ya elimu inatia nguvu hasa kwenye mjadala kuhusu corona. "Journals" sasa hivi zinachomeka "special issues" ili tu kutoa mwanya kwa watu kuandika kuhusu corona. Ajabu taasisi zetu za elimu ya juu, zimekalia tu kutengeneza madishi ya kuoshea mikono, sanitizers na barakoa!
 
Enzi za Nuhu na Safina watu wabishi dizaini yako walikuwepo...

Yaani walikuwa hawaamini kabisa walipokuwa wanaambiwa kuwa Mungu kasema anakwenda kuingamiza dunia nzima kwa maji ya mvua kubwa ambayo haijawahi kutokea huku akiwaleza cha kufanya kwa kila anayetaka kuokoka....

Kwa ubishi wao na kutokutii na kutokujali, matokeo yake ni kuwa wote waliangamia na mtu mmoja tu yeye na familia yake pekee waliotii ndiyo walio okoka wengine wote wakaangamia kwa maji.....

Ishu ya Korona si ya kawaida. Ni "wake up call" toka kwa Mungu mwenyewe ili kurekebisha akili na tabia za watu na kuwafanya waelewe kuwa pasipo yeye Mungu hawawezi kujiponya....

Korona whether we like it or not inakwenda kubadili kabisa mfumo wa maisha ya watu duniani....

Maisha hayawezi tena kuwa sawa na tulivyozoea miaka na siku za nyuma....

Rais John Pombe Magufuli yuko sahihi ktk jambo moja tu na hilo hata mimi nampongeza sana....

Ni la kutambua kuwa yupo Mungu Yehova mwenye nguvu na uwezo wa yote na kwamba huyo ndiye awezaye kumwokoa kila mtu iwapo atamwomba na kumpa maisha yake yote...

Lakini wokovu hauji kwa kuendelea kuwa na aina na staili ya maisha yaleyale tuliyozoea ya dhambi, maisha ya kumchukiza Mungu na kutomtii hata kama tutaomba huku tukipigiza vichwa kwenye mawe na kujichana chana kwa nyembe na visu....

Wanaopona na watakaopona na kifo cha Corona ni wale pekee wanaojinyenyekesha kwa Mungu Baba Yehova na kumheshimu na kumtii yeye pekee yake...

Wengine wote watapiga kelele na kujifanya kwa unafiki tu kuwa wanampenda Mungu Yehova huku mioyo yao ikiwa mbali naye, lakini kamwe, Corona haitawaogopa watu wa namna hii...

Haiwaogopi na itakuwa inawapitia na kuwaua mmoja mmoja kama moto utafunao nyasi kavu uwandani mpaka pale watakapogeuza nyuso zao kumuelekea/tazama Yehova....

Wimbo wa "....maombi, maombi, maombi...." hautamsaidia mtu awaye yeyote kama moyo wake mtu huyo umejaa "chachu" ya dhambi bila kujali mtu huyo ni nani....

Ni bora sana watu hao wakatumia njia za kibinadamu kujiokoa wenyewe na Corona ili ingalau waweze ku - extend siku zao kidogo za kuishi hapa duniani....

Hii ndiyo "logic" iliyo ndani ya kile kisemwacho na kinachoshauriwa na kina Zitto, Mbowe na wengine kitu ambacho siyo kibaya na ni jukumu la serikali yeyote kuwalinda wananchi wake....

Tukirudi kumjadili Rais Magufuli, ni kuwa;

Amewahimiza watu sana waelekeze sauti na nyuso zao kwa Mungu Yehova kwa maana ndiye pekee awezaye kutuokoa. Hilo ni jambo jema sana kwa Rais kuwa na ufahamu huu....

Haieleweki if it's just coincidence ama Mungu kaamua mwenyewe kumtumia bila hata yeye kujua kuwa anatumiwa kama "kipaza sauti cha Mungu" ili yeye Mungu aokoe watu wake.....

Hii inathibitishwa na kitu kimoja, kuwa, Rais Magufuli ana tatizo lake binafsi kama binadamu....

Yeye personally anaabudu miungu yake mingine tusioijua sisi. Utamgundua kwa kauli na matendo yake....

Anahimiza watu waombe Mungu wa kweli - Yehova, lakini yeye mwenyewe akiwa anachanganya changanya ya MUNGU (kwa kusema kwa mdomo), lakini wakati huohuo MOYO WAKE unaamini na kutenda vinginevyo...!!

Mfano huyu Rais anahusudu na kupenda ushirikina wa kujifukizia huku akiwa amejichimbia Chato...

Hivi tunadhani alikuwa anafanya nini kwa zaidi ya siku 50 huko Chato kijijini kwao ili hali hayo ni makazi ya wazazi wake na yeye mwenyewe binafsi..!!??....

Akili kumkichwa....

Kwa hili Mungu Yehova wala hana shida naye, bali adhabu yake kama binadamu wengine ipo juu yake mwenyewe....

Hataikwepa "unless" atambue kosa lake mapema, anyenyekee, atubu na kumwabudu Mungu wa PEKEE, wa KWELI katika Yesu Kristo....!!

Hapo naye ATAPONA....!
Mkuu Kitaturu, kongole sana,kwa mara nyingine tena,umeutendea haki uumbaji wako,na hakika uliumbwa kwa mfano wa Mungu Mwenyezi,Jehova Rapha,Yahweh,Alfa na Omega.
Laiti kama macho yasomayo haya maandiko yako,na ubongo uchakatao haya maandiko,vingefuata haya maandishi,tungekuwa sehemu salama kabisa.
Wenye mamlaka nawaomba mpite hapa mjifunze kitu.
Mungu akubariki.
 
Hao watu 3% wamekufa wapi? Watu wote wa mkoa wa Njombe wafe afu hali iwe kama ilivyo, Subutuuu.

Kwa hili, nampongeza Raisi, he was a visionary.

Sent using Jamii Forums mobile app
100% naunga mkono Zitto ni mchochezi na msaliti wa Taifa. Hivi huyu kimbelembele haoni juhudi kubwa zilizofanya? Anataka nini? Haya wewe Msaliti wa taifa na pia wanasema ni kigagula kweli kweli soma hapa juhudi za zilizofanyika:

1. Kufunga shule na vyuo.
2. Kutia moyo na kutuondolea hofu kuwa koona ni kaugonjwa kadogo.
3. Kuomba tufanye maombi ya siku 3 koona iishe.
4. Wizara ya Afya imefanya siku moja ya kitaifa ya kuombea koona.
5. Imepima koona kwenye mapapai, kwale, mbuzi na oil
6. Imesitisha taarifa ya koona kuwakomoa mabeberu
7. Kimetanza kujifukizia/nyungu
8. Imepeleka ndege kufuata dawa ya asili ya koona Madagascar
9. Imesisitiza watu kutumia vitunguu swaumu, ndimu, malimao n.k
10. Imefunga mipaka na Kenya kuzuia hujuma ya utalii.

Yote haya Zitto huyaoni unataka nini tena??
 
Back
Top Bottom