Enzi za Nuhu na Safina watu wabishi dizaini yako walikuwepo...
Yaani walikuwa hawaamini kabisa walipokuwa wanaambiwa kuwa Mungu kasema anakwenda kuingamiza dunia nzima kwa maji ya mvua kubwa ambayo haijawahi kutokea huku akiwaleza cha kufanya kwa kila anayetaka kuokoka....
Kwa ubishi wao na kutokutii na kutokujali, matokeo yake ni kuwa wote waliangamia na mtu mmoja tu yeye na familia yake pekee waliotii ndiyo walio okoka wengine wote wakaangamia kwa maji.....
Ishu ya Korona si ya kawaida. Ni "wake up call" toka kwa Mungu mwenyewe ili kurekebisha akili na tabia za watu na kuwafanya waelewe kuwa pasipo yeye Mungu hawawezi kujiponya....
Korona whether we like it or not inakwenda kubadili kabisa mfumo wa maisha ya watu duniani....
Maisha hayawezi tena kuwa sawa na tulivyozoea miaka na siku za nyuma....
Rais John Pombe Magufuli yuko sahihi ktk jambo moja tu na hilo hata mimi nampongeza sana....
Ni la kutambua kuwa yupo Mungu Yehova mwenye nguvu na uwezo wa yote na kwamba huyo ndiye awezaye kumwokoa kila mtu iwapo atamwomba na kumpa maisha yake yote...
Lakini wokovu hauji kwa kuendelea kuwa na aina na staili ya maisha yaleyale tuliyozoea ya dhambi, maisha ya kumchukiza Mungu na kutomtii hata kama tutaomba huku tukipigiza vichwa kwenye mawe na kujichana chana kwa nyembe na visu....
Wanaopona na watakaopona na kifo cha Corona ni wale pekee wanaojinyenyekesha kwa Mungu Baba Yehova na kumheshimu na kumtii yeye pekee yake...
Wengine wote watapiga kelele na kujifanya kwa unafiki tu kuwa wanampenda Mungu Yehova huku mioyo yao ikiwa mbali naye, lakini kamwe, Corona haitawaogopa watu wa namna hii...
Haiwaogopi na itakuwa inawapitia na kuwaua mmoja mmoja kama moto utafunao nyasi kavu uwandani mpaka pale watakapogeuza nyuso zao kumuelekea/tazama Yehova....
Wimbo wa "....maombi, maombi, maombi...." hautamsaidia mtu awaye yeyote kama moyo wake mtu huyo umejaa "chachu" ya dhambi bila kujali mtu huyo ni nani....
Ni bora sana watu hao wakatumia njia za kibinadamu kujiokoa wenyewe na Corona ili ingalau waweze ku - extend siku zao kidogo za kuishi hapa duniani....
Hii ndiyo "logic" iliyo ndani ya kile kisemwacho na kinachoshauriwa na kina Zitto, Mbowe na wengine kitu ambacho siyo kibaya na ni jukumu la serikali yeyote kuwalinda wananchi wake....
Tukirudi kumjadili Rais Magufuli, ni kuwa;
Amewahimiza watu sana waelekeze sauti na nyuso zao kwa Mungu Yehova kwa maana ndiye pekee awezaye kutuokoa. Hilo ni jambo jema sana kwa Rais kuwa na ufahamu huu....
Haieleweki if it's just coincidence ama Mungu kaamua mwenyewe kumtumia bila hata yeye kujua kuwa anatumiwa kama "kipaza sauti cha Mungu" ili yeye Mungu aokoe watu wake.....
Hii inathibitishwa na kitu kimoja, kuwa, Rais Magufuli ana tatizo lake binafsi kama binadamu....
Yeye personally anaabudu miungu yake mingine tusioijua sisi. Utamgundua kwa kauli na matendo yake....
Anahimiza watu waombe Mungu wa kweli - Yehova, lakini yeye mwenyewe akiwa anachanganya changanya ya MUNGU (kwa kusema kwa mdomo), lakini wakati huohuo MOYO WAKE unaamini na kutenda vinginevyo...!!
Mfano huyu Rais anahusudu na kupenda ushirikina wa kujifukizia huku akiwa amejichimbia Chato...
Hivi tunadhani alikuwa anafanya nini kwa zaidi ya siku 50 huko Chato kijijini kwao ili hali hayo ni makazi ya wazazi wake na yeye mwenyewe binafsi..!!??....
Akili kumkichwa....
Kwa hili Mungu Yehova wala hana shida naye, bali adhabu yake kama binadamu wengine ipo juu yake mwenyewe....
Hataikwepa "unless" atambue kosa lake mapema, anyenyekee, atubu na kumwabudu Mungu wa PEKEE, wa KWELI katika Yesu Kristo....!!
Hapo naye ATAPONA....!