Kosa ambako nikilikumbuka ninacheka

Kosa ambako nikilikumbuka ninacheka

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nikiwa kama trainee tumetoka field kufika ofisini kila mtu alikuwa na hamu ya kikombe cha chai. Mimi nikiwa mdogo kuliko wote na pia watu hawa ndiyo wa kuni sainia kitabu changu nilizama jikoni.

Nilikuta kibakuli kukiwa na miliyodhani kuwa ni sukari kumbe ilikuwa chumvi. Bidada nikajitosa na tray nikaweka vikombe vizuri na kuwapelekea chai masupervisor wangu.

Walihamaki lakini walijua kulikuwa kosa genuine. Siku wananiaga waliniambia kuwa mwangalifu katika kupambanua chumvi na sukari.
 
Umenikumbusha kitu. .... (dogo) kila akiona sukari nyeupe anadhani chumvi.
 
Ndo tatizo yakununua vitu kwenye mifuko ya rambo...no lebel provided
 
Back
Top Bottom