Mm nikiwa nasoma shule ya msingi nilikuwa sivai sweta msimu wa baridi alafu na yeye aliweka bidii ya kununua masweta ya kila aina..(1996-2002) ilikuwa kulee Tukuyu Mbeya...yaani wakati wengine wanaweka mawe Kwenye moto alafu likipata moto wanachukua wanalishika mkononi alafu safari ya kwenda shule inaanza...kuanzia miezi ya 5 hadi wa 8. alafu mm nikawa sivai aweta na sishiki mawe ya moto.....aisee tunatoka mbali. Kuna mda nikichapwa sana..nilikuwa navaa pale nyumbani ila nikitoka kidogo nalivua nikitoka shule kurudi nyumbani nikawa nalivaa nikikaribia kufika nyumbani..wale wambea wakawa wanamwambia mama mwanao havai sweta shuleni ila akikaribia kufika nyumbani analivaa...basi ikawa fimbo tu....hahahahaa!... Jamani ile baridi ya zamani kule Mbeya naona siku hizi hamna.....masweta sivai hadi sasa yaani hata baridi liweje huwezi kunikuta nmevaa