Kosa gani ulimfanyia mama yako hadi likasababisha akuchape au kukuadhibu?

Kosa gani ulimfanyia mama yako hadi likasababisha akuchape au kukuadhibu?

Mm nikiwa nasoma shule ya msingi nilikuwa sivai sweta msimu wa baridi alafu na yeye aliweka bidii ya kununua masweta ya kila aina..(1996-2002) ilikuwa kulee Tukuyu Mbeya...yaani wakati wengine wanaweka mawe Kwenye moto alafu likipata moto wanachukua wanalishika mkononi alafu safari ya kwenda shule inaanza...kuanzia miezi ya 5 hadi wa 8. alafu mm nikawa sivai aweta na sishiki mawe ya moto.....aisee tunatoka mbali. Kuna mda nikichapwa sana..nilikuwa navaa pale nyumbani ila nikitoka kidogo nalivua nikitoka shule kurudi nyumbani nikawa nalivaa nikikaribia kufika nyumbani..wale wambea wakawa wanamwambia mama mwanao havai sweta shuleni ila akikaribia kufika nyumbani analivaa...basi ikawa fimbo tu....hahahahaa!... Jamani ile baridi ya zamani kule Mbeya naona siku hizi hamna.....masweta sivai hadi sasa yaani hata baridi liweje huwezi kunikuta nmevaa
 
hahaha...nadhani mama alikupa ulichostahili ase......
NILIPATA KICHAPO SANA. NIKAAMRISHWA KWENDA KUBEBA. tena palikuwa na pori na mvua ilishanyesha. kwa bahati nzuri nilifanikiwa kumshawishi mdogo wangu wa kike ili akanitwishe zile kuni. tangu hapo sikuleta mzaha tena.

my mother means everything to me. from birth, motherly care, lessons, guides and advice
 
hahaha....mama yenu alikuwa kauzu mbayaa ase,ulipona sana bhas vipigo ivooo
Mzee alikuwa anakupiga kwa jicho tu unajua hapo umebugi tatizo bimkubwa duh alikuwa moto dogo alichezea sana kichapo cha nguvu. Siku hizi tukikaa nae kama sio yeye amekuwa rahiim kabisa
 
Nilimtishiaga mdogo wangu mtoto wa mamkubwa kumchoma mkuki nilipomkuta kaharibu gari yangu enzi za utoto.

Kuna kipnd baba alinambia pesa ya matumizi atakuwa ananipa mm ninunue matumizi maana akimpa mama haitafika kunako na Mimi nikafanya kama baba alivyoagiza mama alipogundua aliumia sana hata Mimi iliniuma sana najuta
Pole mkuu mimi nimeumia pia.
 
Kama home hawajapika wali na maharage kuoga kwangu ilikua ishu,,,nikiona tu ugali nasingizia kuumwa naenda kulala bila kuoga,lakin ukipikwa punga naoga hata kabla jion haijafika na sotoki home hata kidgo,,bas tabia ya kutokuoga nilikua napigwa kila siku
 
Mm nikiwa nasoma shule ya msingi nilikuwa sivai sweta msimu wa baridi alafu na yeye aliweka bidii ya kununua masweta ya kila aina..(1996-2002) ilikuwa kulee Tukuyu Mbeya...yaani wakati wengine wanaweka mawe Kwenye moto alafu likipata moto wanachukua wanalishika mkononi alafu safari ya kwenda shule inaanza...kuanzia miezi ya 5 hadi wa 8. alafu mm nikawa sivai aweta na sishiki mawe ya moto.....aisee tunatoka mbali. Kuna mda nikichapwa sana..nilikuwa navaa pale nyumbani ila nikitoka kidogo nalivua nikitoka shule kurudi nyumbani nikawa nalivaa nikikaribia kufika nyumbani..wale wambea wakawa wanamwambia mama mwanao havai sweta shuleni ila akikaribia kufika nyumbani analivaa...basi ikawa fimbo tu....hahahahaa!... Jamani ile baridi ya zamani kule Mbeya naona siku hizi hamna.....masweta sivai hadi sasa yaani hata baridi liweje huwezi kunikuta nmevaa
Hahah..asee.sema nin mkuu barid bado ipo t sana,huko mbeya hasa maeneo ya tukuyu.
 
Back
Top Bottom