Kosa kubwa analifanya Rais nikudharau hata wale wamemfikisha alipo je atadumu?

CHADEMA Mungu awasaidie.
Tume huru idaiwe mapema Tanzania
Watanzania hampo salama nawaambia
 
Mkuu ilaumu tume ya uchaguzi. Over
 
Jamani ninaomba kama kuna mtu mwenye clip ya ile dua iliyosomwa pale Jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni za UKAWA, nini kitampata mtu atakayeshinda kwa kuiba kura.
 
Fitina alofanya mstaafu jk kwa viongozi walomfikisha kwenye urais yalimgharimu sana tena sana miaka kumi baadaye...sasa huyu naye anafanya kosa lilelile alofanya mtangulizi wake...ilibaki kidogo sana ccm imfie jk 2010 kwa sababu ya dhambi kam hii hii inayofanywa sasa....hivyo tutegemee anguko kubwa sana tena la kishindo 2020 kwa ccm....Hakika MWENYENZI MUNGU AKITAKA KUMUANGAMIZA MWANADAMU HUMPOFUSHA ASIONE LITAKALO MPATA MBELE.....CCM wamepofushwa.
 
CCM haina jema kwa nchi hii. Wengine tulisema sana kuwa licha ujio wa ghafla wa Lowassa UKAWA 2015 (nikiri kuwa mimi ni mmoja wa waliosikitishwa na mambo yale) lakini nilitafakari na kupima na kuona kuwa bado haikuwa sababu ya kuisaliti nchi yangu, bado haikuondoa uhalali na sababu za kuitoa CCM madarakani. Bahati mbaya wengi walishindwa kurudi kwenye utulivu wa fikra na kuishia kupiga kura za hasira na kukomoa; lakini ilitupasa tuone mbali zaidi ya hisia zetu na tofauti zetu.

Sasa wananchi wenzangu, ikifika 2020, chonde chonde wananchi tuweke mbali tofuati zetu tuitoe CCM. Ziko faida na sababu nyingi mno za kuitoa CCM vs za kuibakisha. Kumbukeni huyu Magufuli ndio the very best CCM had to offered us. Imagine this very John is their best lot! Nitoe mifano/sababu chache tu:-

1) Baada ya kuing'oa CCM tutakuwa tumeweka msingi (precedence) kwa chama tutakachokipa dola kuwa tunataka maendeleo na sio uhuni uhuni kama sasa. Na wakishindwa kutupa mahitaji watakuwa wamevunja mkataba na tutawatoa kwenye mamlaka kama tulivyoitoa CCM.

2) Itakuwa ni rahisi kubadili utawala na sheria za nchi pale tutakapoona (wananchi) inahitajika. Tutakuwa tumevunja kuhodhi (monopoly) ambako CCM imejimilikisha kama ilivyo sasa. Yaliyofanyika kwenye mchakato na Bunge la Katiba 2015 ni aibu ya kihistoria na ufisadi wa kiwango cha lami, lakini ile ndio CCM halisi katika ubora na rangi zake.

3) Tutakuwa tumevunja mwiko (mental barrier) ya kuwa bila CCM kutakuwa na vurugu pamoja na upuuzi mwingine wenye kufanana na huo.

4) Tutajenga wigo mpana wa ushiriki na mkusanyiko wa mawazo na hoja zenye tija badala ya siasa mfu za ki-CCM.

5) Kwa mara ya kwanza umiliki wa nchi na Taifa utakuwa mikononi mwa wananchi badala ya genge la wachache CCM.

6) Kama ilivyokuwa punde baada ya uhuru mwaka 1961, wananchi watajawa na ari na mwamko mpya wa nchi yao. Watajitoa na kushiriki kwa hiari kuijenga na kuipigania nchi yao tofauti na ilivyo sasa.
 
Haijarishi,ukitumika unakwenda na maji[emoji16][emoji16]
 
Haka ni kasayari kapya tunaishi kamegunduliwa na mfalme na mwanamfalme. Hata namba zake bado sijazielewa natakiwa nizisomaje. Hii ni zaidi ya ccm ileile/mbele kwa mbele.
 
There is karma and is real!.
Paskali
 
Kwa nini asidumu wakati ccm wameishabadili mtazamo mapema tu kuwa 2020 asiwe na mpinzani au mgombea urais yaani apite ndani ya chama moja kwa moja bila kura.
Wengi hawakulielewa hili, sasa litaeleweka. Ukitaka mengineyo 2020 ujaribu nnje ya CCM au sivyo usubiri 2025 ukiwa ndani ya CCM otherwise ugombee ukiwa nnje.
 
Wengi hawakulielewa hili, sasa litaeleweka. Ukitaka mengineyo 2020 ujaribu nnje ya CCM au sivyo usubiri 2025 ukiwa ndani ya CCM otherwise ugombee ukiwa nnje.
Haswa kwani Lisu alishawaambia hii ni serikali ya aina gani watu mkaguna sasa ndo muone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ