Kosa kubwa la wamasai ni lipi?

Kosa kubwa la wamasai ni lipi?

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Ndani ya nchi yetu kumekuwepo na ubaguzi wa wazi dhidi ya watu wa kabila la wamasai.

Imekuwa ni kawaida kuwaona na kuwatambua watu wote Kama Watanzania isipokuwa maasai ndio hutambulika Kama wamasai.

Kwanin tunatumia utambulisho wa kikabila Kwa maasai Ila Kwa wengine tunatumia utambulisho wa Utanzania?

Mathalani utasikia mlinzi wa kimasai au kijana wa kimasai lakin huwez sikia mlinzi wa kinyakyusa au kisukuma.
Screenshot_2024-07-21-12-46-54-580_com.facebook.katana.jpg
 
Wamejitenga.

Wapo kienyeji zaidi wanashikilia sana mila zao ndo maana wanaonekana kama wageni.

Halafu ubaya ni kwamba hata hawafaidiki, wanatangaza utalii lakini pesa zinaenda kwa wengine, hawatajiriki.
 
Ndani ya nchi yetu kumekuwepo na ubaguzi wa wazi dhidi ya watu wa kabila la wamasai.

Imekuwa ni kawaida kuwaona na kuwatambua watu wote Kama Watanzania isipokuwa maasai ndio hutambulika Kama wamasai.

Kwanin tunatumia utambulisho wa kikabila Kwa maasai Ila Kwa wengine tunatumia utambulisho wa Utanzania?

Mathalani utasikia mlinzi wa kimasai au kijana wa kimasai lakin huwez sikia mlinzi wa kinyakyusa au kisukuma.View attachment 3047808
Ni watu maarufu sana.
Hata wasukuma nao hutambulika hivyo hasa wale wa porini.
Masai wana life style yao. Wabantu tulishavurugwa na wazungu na warabu. Hatuna utamaduni hivyo tunaonekana tofauti na Masai .
 
Ukitembea mapaja nje watuu wanakushangaa ila masai hamshangai
Ukitembea na sime au kisu mtaani watu wanaulizana kulikoni ila siyo masai
 
Wabantu sisi ni watu wabaya sana, tena wabinafsi. Ona Hadzabe walivyoathiriwa na wabantu.
Wabantu hatujali maisha ya hayo makabila. Wabantu ndio makabila yanayomiliki ardhi kubwa TZ lakini bado tunadhulumu wahazabe na wamasai. Kwa nini ?
Nani anawatetea hao watu ?
Wamasai ni wa kupongeza na ni watu Imara wasioyumbushwa na fikra za kimagharibi japo baadhi yao wameanza kuiga maisha ya wabantu.
Masai mkiiga maisha yetu mtakuwa wafupi, vitambi, stress, wanafiki nk.
Shauri yenu.
 
Back
Top Bottom