Kosa kubwa la Yanga ni kujifananisha na Simba!

Kosa kubwa la Yanga ni kujifananisha na Simba!

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Simba atabaki kuwa Simba kwenye michuano ya kimataifa na yanga wazee wa ndondo cup watabaki kuwa yanga.

Kosa kubwa hapa yanga wanataka kuifananisha timu yao na Simba kwenye mafanikio ya kimataifa ili hali timu yao ni changa, malengo ya hersi ilikuwa ni group stage na wamefika ila mashabiki wa utopolo huwa hawana kumbu kumbu kama kuku, hapa wameanza kujipa matumaini kwa kupiga hesabu za vidole kwa kusema watashinda mechi zote kwa mkapa japo jambo hilo ni gumu mzunguko wa kwanza wamepiga moja wajue wakabisa watapasuka tena japo game moja amma mbili.

Mechi ya Mazembe tumeona kila hatua timu ya yanga ni ile ile Mazembe katoka sare na Aligers kapigwa na Hilal katoka sare na yanga.

Hesabu za vidole wamepigwa na Hilal wakapigwa na Algers wame droo na Mazembe kimatokeo wanafanana ndio timu mbili mbovu kwenye kundi inashangaza wakijinasibu kupita kwenye hilo kundi sijui kwa mpira gani na uwezo gani kiwango kipi na wachezaji wapi.

Simba siku zote wanapindua meza huwa wana wachezaji wenye kujituma na wanajua nini wanchokifanya tayari wachezaji wa simba wamejengwa mashindano ya kimataifa wao ndio wawakilishi pekee wa taifa la Tanzania.

Yanga hawatafuzu hili kundi kwa kujifanananisha na Simba hawana timu ya kushinda mechi zote.....mtanikumbuka!
 
Simba atabaki kuwa Simba kwenye michuano ya kimataifa na yanga wazee wa ndondo cup watabaki kuwa yanga......
Kosa kubwa hapa yanga wanataka kuifananisha timu yao na Simba kwenye mafanikio ya kimataifa ili hali timu yao ni changa....malengo ya hersi ilikuwa ni group stage na wamefika ila mashabiki wa utopolo huwa hawana kumbu kumbu kama kuku.....hapa wameanza kujipa matumaini kwa kupiga hesabu za vidole kwa kusema watashinda mechi zote kwa mkapa.......japo jambo hilo ni gumu mzunguko wa kwanza wamepiga moja wajue wakabisa watapasuka tena japo game moja amma mbili......
Mechi ya Mazembe tumeona kila hatua timu ya yanga ni ile ile Mazembe katoka sare na Aligers kapigwa na Hilal katoka sare na yanga......Hesabu za vidole wamepigwa na Hilal wakapigwana Algers wame droo na Mazembe kimatokeo wanafanana ndio timu mbili mbovu kwenye kundi inashangaza wakijinasibu kupita kwenye hilo kundi sijui kwa mpira gani na uwezo gani kiwango kipi na wachezaji wapi......Simba siku zote wanapindua meza huwa wana wachezaji wenye kujituma na wanajua nini wanchokifanya tayari wachezaji wa simba wamejengwa mashindano ya kimataifa wao ndio wawakilishi pekee wa taifa la Tanzania.......yanga hawatafuzu hili kundi kwa kujifanananisha na Simba hawana timu ya kushinda mechi zote.....mtanikumbuka!
Yanga sio bure mpira wao umebadilika ghafla sio yanga ile waseme ukweli hawa walikuwa wanajidunga syringe isee!
 
Yanga sio bure mpira wao umebadilika ghafla sio yanga ile waseme ukweli hawa walikuwa wanajidunga syringe isee!
umeangalia mpira wa Tp , umeangalia umiliki wa yanga na kufika golini ama bado unatembea na kauli hizo za kujifariji

man city nae kashuka kiwango vipi alikuwa anatumia sindano.
 
Mwenzio kacheza fainali Caf wewe badala ukomae umfikie unapiga domo na mwenzip yupo club bingwa!
Inategemea una umri gani, Simba kacheza fainali ya Kombe la CAF, hiyo hapo ticket ya mechi.
 

Attachments

  • Screenshot_20241215-082240.png
    Screenshot_20241215-082240.png
    2.1 MB · Views: 7
Simba ilitakiwa icheze michezo ya ndani tu kiukweli hata weye ulieandika huu uharo unalijua hilo ila huwa mnajichetua kwa kusema sijui watani wa jadi(Hapo mnavyokua mnatafuta huruma na kujifananisha na yanga)ila ukweli mchungu ni kwamba yanga sio level zenu amekuwa akiwachenyenta mfulululizo kila mkimsogezea kalio mbusi nyie kuweni na adabu
 
Mkuu kipara kipya kuwaita yanga kuwa ni timu ni kupoteza muda wale ni wahuni waliojikusanya na kuanza kucheza Mpira kama sehemu ya misheni ya kutakatisha fedha na Dili zingine nyeusi. GSM wameondoa kipengere Cha wanachama ili wabaki na Siri zao.
 
Back
Top Bottom