Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 42
Mawazo ya kupata mahitaji ya wananchi katika kuunda Ilani za vyama na kusimamia utekelezaji wake ni jambo zuri sana. kinachotakiwa ni namna ya kuweza kusimamia na kutengeneza hizo ilani. Kuundwa kwa chombo kitakayoshughulikia uundwaji wa ilani hizo.
Matatizo yanayoweza kujitokeza ni kama yafuatayo:
1. Tofauti za kiitikadi za vyama vya siasa: Vyama vya siasa hutoa ahadi zao kulingana na itikadi zao na hasa jinsi vinavyoona/amini na kujipanga kutekeleza mambo mbalimbali wanayoahidi kuyatekeleza endapo watachaguliwa.
2. Muda mrefu utahitajika ili kuweza kuunda, kukusanya na kutengeneza Ilani hizo, na baadae kuzipeleka kwa wananchi kwa uhakiki kabla ya kuelimisha vyama vya siasa kwa ajili ya makubaliano ya kuwa ilani kamili.
3. Itahitajika umakini mkubwa katika uandaaji wa makundi ya wananchi ili kuweza kufikia lengo linalokusudiwa, kwa muda unaotegemewa na kwa ubora stahiki. Elimu kwa waanchi juu ya malengo/matarajio ya ilani hizo ni jambo muhimu sana.
4. Udanganyifu wa vyama kuhusu utekelezaji wa ilani hizo za wananchi. Ni rahisi zaidi kwa kila chama kuahidi kuwa kina uwezo wa kutekeleza mapendekezo yote ya ilani za wananchi, na hiyo kuwa kinyume wakati wa utekelezaji. Hivyo ni rahisi kuchagua serikali iliyodanganya na itakayodai kuwa ilani haikutekelezeka na haikuwa yao.
Kwa muda mrefu (tangu tuanze kuwa na chaguzi za vyama vingi vya siasa), vyama vimekuwa vikitengeneza Ilani zao na kuzisoma kwa wananchi wakati wa kampeni. Wananchi hawajawahi kupata nafasi ya kutosha kupitia ilani hizo na kuzitolea maoni yao. Nadhani si vibaya vyama vikaunda ilani. Ila ni vyema zaidi ilani zikasambazwa na kupatikana mapema ili wapiga kura (wananchi) waweze kuzichambua na kuzielewa ili waweze kufanya maamuzi mazuri katika uchaguzi.