Uchaguzi 2020 Kosa kubwa walilofanya CCM kwenye kampeni zao ni kupoteza muda kusifia yaliyopita badala ya kueleza watafanya nini

Uchaguzi 2020 Kosa kubwa walilofanya CCM kwenye kampeni zao ni kupoteza muda kusifia yaliyopita badala ya kueleza watafanya nini

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watachaguliwa tena.

Kwenye kampeni zao mara nyingi utawasikia tumejenga hiki, tumenunua hiki, tumejenga flyover, tumenunua ndege, tume... tume... zilikuwa nyingi, vitu ambavyo tayari watu wanavijua, inaboa, ndio maana baada ya wasanii kumaliza watu walikuwa wanaondoka kwa sababu wanajua wataambiwa yaleyale ya jana, nashangaa kwanini kampeni meneja alikuwa haja notice hilo.

Tofauti na Chadema ukienda kwenye kampeni zao walikuwa wanasema mkituchagua tuta fanya hiki, tutabadili hiki... tuta... tuta... hadi hotuba inaisha bado unawaacha watu na hamu ya kusikiliza wakidhani labda utasema kingine kipya.

Kampeni ni tofauti na hotuba au mahubiri ya kanisani ambapo waumini wanajua lazima utawaambia juu ya Yesu kurudi, kampeni ni technique ushawishi sio kutumia nguvu na kulazimisha watu wakusikilize, matendo kama ya kina Sabaya hayaongezi kura badala yake yanajenga chuki na kuipunguzia kura CCM.
 
Haya ni matokeo tu ...Wapambe wa JPM walishindwa kuelewa kuwa Uongozi Ni kushawishi! Inategemea unashawije!
Wao waliamua (JPM)? kutumia nguvu na hila.

Mtindo huu unatanya/ ilikuwa unatanya kazi kwenye Jamii zilizotopea ujinga,kukosa taarifa!

Hata ndani ya mtindo huu lazima uwe na Timu mahiri yenye weledi ...inayotumia akili!

Kipindi fulani Vyama vya Kijamaa vilifanikiwa katika hili! Ni kuwafanya watu Wajinga kuwaambia ...Maendeleo hayanan Chama ,kesho unaeaambia mkichagua Upinzani siwapi maji.

Watu kwa kuwa wameumbwa na silika wanaweza kuamua kuchagua kukosa maji (ndicho kinachotokea Sasa) ilinwskuoneshe tu kuwa wao Binadamu kamili wanaohitaji kutambuluwa na kuheshimiwa utu wao.

CCM inahitàji watu jasiri kwa Sasa kusema no,la sivyo just linawapa mgongo.
 
Na lazima tumuondoe kwa Lazima au kwa hiari. Kwa mfano alivokua shinyanga na Bunda alikua akilazimisha watu kwa nguvu kuwa msipowachagua wabunge wa Ccm sita leta maendeleo kwenye majimbo yenu.

Alivoenda Kawe kwa Alima mdee alazimisha watu wamletee gwajima akidai maendeleo hayana vyama. Magufuli ni fungu la kukosa hana jipya.

Bashiru na polepole wanamdanganya,ukichanganya na ukichaa wake lazima tumuondoe kwa lazima.
 
Lisu ni mpango wa Mungu, hayo yote lazima yatokee ili kuwepo na utimilifu wa neno la Nyerere, kwamba, wakuitoa ccm ni ccm wenyewe,
Nimeamini maneno hayo kwani naona kabisa akina
@Hpolepole
@AllyBashiru
@KheriJames
@DkMagufuri
@DcSabaya

Ndiyo wataiangusha ccm kwa vimbwanga wanavyovionyesha wazi na vimeongeza chuki kwa wananchi
 
CCM walikua wanasafisha njia kwa uongo na ulahai wenu mlowalisha wananchi katika kampeni.

Kwamba ndege,ujenzi wa nchi,maendelo ya vitu hayaitajiki nchi hii.

Hapo ndo watu wakawaona nyinyi kweli Ni mwezi mchanga
 
Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER). CCM sio wajinga wapo jikoni wanaset mitambo wakati nyie mmekazana na Mambo yasiyo na impact mpo bize kushangilia helicopter aliyokodi Lissu. Kwa akili hizi za kujipa moyo CCM itaondoka madarakani miaka 50 ijayo.
 
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamepoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watawachagua tena...
Nani alikuambia CCM wana akili? Kwa ubongo ipi? Na uongozi upi? Haya majamaa yaitwayo Bashiru, Polepole, na Jiwe ndiyo think tanks za chama? Utasubiri sana.
 
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference.

Tangu kampeni zianze CCM wamepoteza muda mwingi kuelezea vitu walivyo fanya wakasahau kuwaeleza wapiga kura nini kipya watawafanyia wananchi endapo watawachagua tena...
Mkuu, Mwenye CCM yake alishasema hapangiwi na wala hashauriwi kwani hakuna aliyemshauri kuchukua form.
 
Kawaida na hulka ya binadamu ni kutamani kusikia au kuona kitu kipya kuliko cha zamani, wazungu wanasema test the difference...
CCM Wanaboa,ni kama staili za mapenzi kitandani,kila siku ile ile tu,mpaka kero...

Walijaribu kuiendesha Tanzania kwa kutumia fikra chakavu na za kijima za mwebyekiti...ona zilipo wafikisha....pathetic
 
Kama mitandao inadanganya,je ule umati unaojaa kwenye mikutano ya Lissu ambao habari za Lissu mnawanyima kuziona kwenye mainstream media habari zake wanazitoa wapi...?
Pathetic
Kwenye mabasi, kwa kinyozi, kwa mama ntilie nk, kila mtu anaangalia clips za Lissu. Huyo anajianika TBC na fly-overs zake hakuna anae angalia.
 
Umesema kweli lakini kuna mijitu inayolipwa kuongea pumba itakuja kukupinga hapa na kukubishia.

ukweli kampeni ni kama kutongoza vile hata mkeo ndani anapenda kuskia ahadi mpya kwamba nitakununulia nguo nitakuletea viatu nitakupeleka movies.

Lakini ukimwambia nilikununulia nguo nilikuletea viatu nilikupeleka movies anakuchoka sababu yale ameshayaona hayana jipya tena kwake.
Big up sana hili andiko ni bora kabisa kwa wenye akili.

Watu wanataka kuskia mambo mapya yajayo siyo yaliyopita.
 
IMG_20201017_221108_276.jpg

Watanzania sio wajinga kusulubisha mleta maendeleo, na kuwaacha mla ruzuku, michango ya wabunge pamoja na kula vitu maalum wazee wa faru John. Genge lenu la wahuni, mwisho Oct 28.
 
Mitano tena ya Bombardier
Mitano tena ya Meli na vivuko
Mitano tena ya barabara
Mitano tena Madaraja
Mitano tena ya Masoko ya kisasa
Mitano tena ya Shule
Mitano tena ya hospitali na vituo vya afya na zahanati
Mitano tena ya kukamilisha SGR
Mitano tena ya SMEs
Mitano tena ya ajira za elimu,afya,fundi mchundo
Mitano tena ya Umeme Imara na vijiji vyote
Mitano tena ya pembejeo za Kilimo
Mitano tena ya chanjo za kizalendo za mifugo
Mitano tena ya miundombinu ya IT
Mitano tena ya Utalii wa kiutamaduni
Mitano tena ya AFCON na World CUP.

KWA CCM UTEKELEZAJI NI AHADI.
CHAGUA JPM
 
Kulikuwa na ndege za FASTJET, Dar - Mwanza ilikuwa sh elfu 70, sasa jiwe kaua Fastjet ameleta madege ya Bombadier ya kinyonyaji, Dar - Mwanza kwa sasa ni sh laki 4, afu jiwe anawadhihaki wanyonge kuwa anawasaidia!
Dar -Mwanza sh 70,000/= to 400,000/=? 😭

---Sukari sh 1,800/= to 2,800/=


Halafu anataka mingine✊🏻?

"Ni mwendo wa ✌🏻✌🏻✌🏻 tu"
 
Hivi sera ya CCM mwaka huu ni IPI? Maana nasikia tu " Mitano tena "
Mitano tena, wacha kazi iendelee. Kazi ya stiglers, standard gauge, madege, umeme vijijini vilivyobaki, hospital, barabara et
Na lazima tumuondoe kwa Lazima au kwa hiari.
Kwa mfano alivokua shinyanga na Bunda alikua akilazimisha watu kwa nguvu kua msipowachagua wabunge wa Ccm sita leta maendeleo kwenye majimbo yenu.

Alivoenda Kawe kwa Alima mdee alazimisha watu wamletee gwajima akidai maendeleo hayana vyama.
Magufuli ni fungu la kukosa hana jipya.
Bashiru na polepole wanamdanganya,ukichanganya na ukichaa wake lazima tumuondoe kwa lazima.
Mwondoeni Mbowe kwa lazima au hiari kwa kula ruzuku na michango ya wabunge 1.5Mil. Magufuli haondoki hata kwa greda. Maana yeye mwenyewe ndo tingatinga na limetinga mpaka Ufipa.Huwezi amini, wengi miongoni mwenu mtampigia kura JPM.
 
Back
Top Bottom