Uchaguzi 2020 Kosa kubwa walilofanya CCM kwenye kampeni zao ni kupoteza muda kusifia yaliyopita badala ya kueleza watafanya nini

Na lazima tumuondoe kwa Lazima au kwa hiari.
Kwa mfano alivokua shinyanga na Bunda alikua akilazimisha watu kwa nguvu kua msipowachagua wabunge wa Ccm sita leta maendeleo kwenye majimbo yenu...
Kiongozi mbaguzi kuwahi kutokea
 
Mbona CHADEMA wanatumia kigezo cha yaliyofanyika kwamba yamefanyika vibaya badala ya kusema watafanya nini....Tuseme tu CCM imewashika pabaya mwaka huu
 
Tumia akili ulizopewa na Mungu vizuri! mbowe kaigiaje hapa? watu wanauliza sera yenu ni ipi?? wewe unaleta ujinga ujinga hapa!! mshamba!!!
 
Kwani wamepoteza muda?
Subiri uone ushindi wao wa kishindo

UKAWA/CHADEMA nafasi ilikuwa 2015 ila kwa kuwa ile ilishindikana... ndio basi tena
 
Robert Amsterdam kawadanganya, mwambieni Magufuli haondoki jana leo hata kesho. Hivyo rudisheni advance ya rasilimali mliochukua.
Kuna swali limulizwa. Wakati jiwe anaingia nauli za fast jet kutoka Dar Mwanza ilikuwa 70,000 tu! sasa ni 400,000!

Sukari ilikuwa 1800tu! sasa ni 3000-3500
MAUZO YA MAZAO
Pamba ilikuwa inauzwa 2500@kg sasa ni 1200 na wanunuzi wote ni makada wa ccm!!

Kahawa ilikuwa inauzwa sh 2500-3000@kg, sasa inauzwa 1200

Kwa kifupi. Magufuli ameua uchumi wa nchi yetu!!! lazima aende!!!
 
Uko sahihi sana, lakini kuongezea kitendo cha kampeni kutawaliwa na sanaa kwa asilimia 80% badala ya Sera ni kosa kubwa kisiasa. Wenye busara wanakuona kama una mizaha na maisha yao.
Kampeni inaanza saa 2 asubuhi ni miziki tu na kupongezana na kutambulishana hadi saa 9 mgombea anapopewa nafasi watu wameshachoka.
 
Wangapi wana ilani ya CCM je wameisoma? najua hata wewe huna.
 
Nani alikuambia CCM wana akili? Kwa ubongo ipi? Na uongozi upi? Haya majamaa yaitwayo Bashiru, Polepole, na Jiwe ndiyo think tanks za chama? Utasubiri sana.
Utaona akili zao baada ya tarehe 28.....uzuri upande mmoja madomokaya upande wa pili ni vitendo tu .......povu ruksa
 
Tatizo ni kuwa CCM hawana jipya la kufanya muhula wa pili tukikosea tena tukawapa kwa sababu wamesema wazi kuwa wapewe miaka 5 mingine wakamilishe Miradi walionza. Hayo yamesemwa na mgombea wao wa Urais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na viongozi wa Chama Chao hii ina maana wamenunua madege 11 cash yamekuja 8 bado 3 wanaomba muhula mwingine madege yote yawasili ATCL ianze kazi. SGR ilikuwa ikamilike hadi Moro mwezi November, 2019 haijafika sasa wanaomba muhula mwingine wafike Moro mwezi Februari, 2021, miradi mingine inayoombewa miaka mingine 5 kumalizia ni pamoja na MGW 2115 za umeme wa Stiegler's Gorge, Uwanja wa ndege Chato, Daraja la Busisi na mingine. Wao ni tumefanya hiki na kile na kile kule mtu akihoji kutaka kuona viko wapi atakamatwa kwa uchochezi au utakatishaji fedha. Tulifanya kosa, tusirudie kosa!
 
Kulikuwa na ndege za FASTJET,
Dar - Mwanza ilikuwa sh elfu 70, sasa jiwe kaua Fastjet ameleta madege ya Bombadier ya kinyonyaji, Dar - Mwanza kwa sasa ni sh laki 4, afu jiwe anawadhihaki wanyonge kuwa anawasaidia!
Kwani lazima upande ndege kama kipato chako cha kuunga unga? Panda najimusa au happy nation wacha kutamani vitu usivyovimudu.

Haya lissu ataleta ndege bila kulipa nauli siyo?
 
Ni SAWA kabisa wanavyofanya CCM. Wao ndio waliopewa dhamana mika mitano iliyopita na ilani yao ndio ilikuwa inatekelezwa. Lazima waeleze kwa kina walivyotekeleza ili waweze kujenga imani ya wanainchi kupewa tena imani yao kwa miaka mitano ijayo
 
Naunga mkono hoja maana yaliyofanywa sio kwamba watu hawayaoni lakini tunahitaji hali zetu zinyanyuke na sio historia. Ingeluwa hivyo Austria walianza kujenga miundombinu vijijini toka 1954 huko na hawaongelei tulijenga daraja hapana watu wanataka kusikia kuhusu ajira, pensheni, mikopo ili kujimwamua kiuchumi wenzetu wanaongelea Interest rate kila siku kwenye taarifa za habari ili kuchochea uwekezaji wa wananchi na mikopo.
 
Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sio 2020 bali ni kamwe (NEVER).
Wananchi ndo wanaamua Nani wamchague utake usitake. Wakimchagua Lissu kwa kura nyingi ww mmoja utafanyaje, utampora ushindi?!
 
Ni SAWA kabisa wanavyofanya CCM. Wao ndio waliopewa dhamana mika mitano iliyopita na ilani yao ndio ilikuwa inatekelezwa. Lazima waeleze kwa kina walivyotekeleza ili waweze kujenga imani ya wanainchi kupewa tena imani yao kwa miaka mitano ijayo
Msemaji Mkuu wa serikali katangaza haya kwa miaka 5, TBC inatangaza na kuonyesha kila siku, kampeni ni zaidi ya kufanya hivyo.
 
Mkuu inakuwaje unatumia post ile ile kila mahali? Umeamua kucopy na paste!

Hapo ni kuishiwa kupitiliza
 
Eti wako jikoni wanaset mitambo

Mipango ya kuiba KURA😜😜😜
 
Hajui hata lissu akijaza uwanja habari zinaanzia wapi
IDIOT kabisa
Hajiulizi kwanini wakubwa zake wanahangaika usiku kucha kumfuta KIGOGO 2014
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…