Kosa la kiufundi la wanaume linalopelekea kupata wenza wasiofaa katika maisha ya ndoa zao!

Kosa la kiufundi la wanaume linalopelekea kupata wenza wasiofaa katika maisha ya ndoa zao!

Yani umeandika point tupu mkuu Uzi nimeuweka Bookmark,

Tatizo ni kwamba ushauri watu wanapewa vzuri kabsa na wanaupokea ila wakitoka online tu kila mtu analudia mapito yake......Wanaume tubadilike.
 
Wanaume wengi wenye pesa huwa hawawajui vizuri wanawake

Ndo maana huwa ndoa zao haziishi changamoto
wahuni ndio tunaenda sawa na wanawake,,,,hata ukiwa na pesa ila sio pesa iliyofanya kazi...wanaume ehhh hap akazi tu
 
Yupo la pili fulani hivi ana isumbua hatari. Hata nikimpa sharti la kumkuta njiapanda saa 4 usiku anatekeleza. Huyu anafaa kuwa mke? Mbona hahoji chochote?
 
"Ndoa Ni pasua kichwa!"

Alisikika mwanaume mmoja akiwa amelewa chakari.

Ndio, Kuna kosa kubwa Sana wanaume tunafanya mwanzoni kabisa!

Kosa la kumshawishi mwanamke ili aingie ktk mahusiano ya mapenzi!

Upendo Ni tunu ya moyo! Iko natural, kamwe haiwezekani kuushawishi upendo!

Kinachowezekana kukishawishi kwa mwanadamu ni matamanio na si upendo

Ni rahisi Sana kumtamanisha mwanadamu

Wanaume tuna desturi ya kujisifu na pia kusifiana uanaume katika kuonesha uwezo wa kutongoza. Vuguvugu hili linaanza ktk teen ages za mvulana

Nyakati hizo vivulana vinaanza kuoneshana ubabe wa kung'oa vibinti virembo mtaani au shuleni.
Vivulana vinapambana kutongoza vibinti vinavyosifika kukataa na anayefanikiwa anaonekana kidume

Hapa ndipo penye kosa la kiufundi!
Wanaume tunachodhani sifa ya uhodari wa kumshawishi mwanamke mrembo au mgumu ndiyo shida inapoanza!

Ni hivi, mwanamke asiyekupenda atakusumbua Sana ktk Harakati za kumtongoza. Utamshawishi kwa sifa ya cheo chako, fedha zako na kumuonesha care za kitapeli, ahadi za uongo uongo, na mwishowe ataingia kwenye kumi na nane!

Utamla na utaamua kumuoa, lakini hio haiondoi fact kwamba deep inside her heart hana upendo

Ndoa ni maisha
Maisha yanasonga na huenda yote ya ushawishi kwa mwanamke wako yanafifia

Cheo kitaondoka, biashara zitayumba, , na Sasa mpo kwenye maisha Yale ambayo hakuna tena msisimko wa furaha za maisha, au yale uliyomshawishi nayo yamekuwa sehemu ya maisha yake na hivyo hayana mvuto tena

Huo Sasa ni muda wa mwanamke kukutenga. Mume na mke munaishi ndani ya nyumba Kama mtu na jirani yake!

Usiku unanyimwa, ukimgusa anakusukuma,

Mukifanya tendo hafiki kileleni kwani wewe si type ya moyo wake

Watoto anawalisha sumu wasikupende,

Makosa madogomdogo ya mume yanakuzwa saana, ili ajikasirishe muda wote

Ukizeeka anakuona kero anakwenda kuishi pamoja na mtoto wake nje ya mkoa

Wanaume tuache kung'ang'aniza mahusiano kwa kutongoza saana na matumizi makubwa ya ushawishi wa kila namna, ili tu upewe sifa ya kung'oa binti mrembo!

Hawa wanawake Wana moyo wa kupenda pia!

Nao wanapenda kwa kumtazama tu Mwanaume kwa mara ya kwanza tu iwe kwenye gari, kwenye semina, kazini na kokote kule wakutanako

Siku zote unakutana nao maeneo mbalimbali na unaweza kubaini yupi yupo interested na wewe!

Sisi wanaume tuna ujinga Fulani eti hatuwapendi wanawake wanaotuonesha wanatupenda
Tunawaita shobo na Malaya!

Katika hili tujilaumu wenyewe kwa kujitengenezea mahusiano ya ndoa kwa wanawake wasiotupenda.
Japo lawama tunawapa wao kuwa wanaingia kwenye ndoa kimkakati ilihali tumewalazimisha kuwaoa kwa vishawishi mbalimbali!

Tuoe wanaotupenda
Tusitafute mapenzi kwa vishawishi.
Ni kazi kweli
 
Yupo la pili fulani hivi ana isumbua hatari. Hata nikimpa sharti la kumkuta njiapanda saa 4 usiku anatekeleza. Huyu anafaa kuwa mke? Mbona hahoji chochote?
Huyo anakupenda sasa.
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Wanaume wengi wenye pesa huwa hawawajui vizuri wanawake

Ndo maana huwa ndoa zao haziishi changamoto
Tatizo ni kuwa kama una mkwanja wa haja wanawake wengi wanakuwa wanataka pesa yako na ku fake upendo, so inakuwa ni rahisi tu kwa mwanaume husika kuangukia mikononi mwa tapeli maana anaigiziwa vigezo vyote vya wife material. Mwisho wake anakuja kugundua hakupata bali alipatikana yeye
 
Tatizo ni kuwa kama una mkwanja wa haja wanawake wengi wanakuwa wanataka pesa yako na ku fake upendo, so inakuwa ni rahisi tu kwa mwanaume husika kuangukia mikononi mwa tapeli maana anaigiziwa vigezo vyote vya wife material. Mwisho wake anakuja kugundua hakupata bali alipatikana yeye
Point ya maana kabisa
 
Back
Top Bottom