Usijali naamini sasa hivi utakuwa tayari umeripoti chuoni maana mwaka wa kwanza mlitakiwa kuripoti tarehe 24 mwezi huu, siku ya kujisajili utapewa kitu kinaitwa course content hapo utapata kujua ni nini utarajia kupata pindi umalizapo kozi hiyo na hapo ndio unaweza jua ni pana kiasi gani. na kwa kuongezea tu siku hizi pale SUA kuna kozi ya Intaprenyuashipu( Enterprenuership) ambayo ni lazima kwa kila mwaka wa kwanza na wa pili so utajifunza ujasiliamali na mbinu zake, so huwezi toka kapa kwa kozi yoyote ile usomayo pale SUA. Kuhusu mchakamchaka wa SUA ninachoweza kukushauri ni kuwa "Utamu wa ngoma ni uingie kucheza" kama wengine wameweza wewe utashindwa nini, ythe fact that umechagulia kujiunga pale SUA it means wewe ni University material so utaweza tu, muhimu ni kukaza buti maana bado una safari ndefu!