Kozi ya Staff Cardet jeshini! Nini hufundishwa huko?

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,385
Reaction score
10,659
Just for learning!

Japo mie ni nazi iliyoivia mtini, ikachumwa na kuuzwa sokoni na sasa mama ntilie anaikodolea macho, napenda kujifunza kitu kuhusu staff cardet na zaidi:

Kwa Tz kijana huanza na JKT kisha akichaguliwa huingia kwa mafunzo ya JWTZ ambapo hufunzwa zaidi mbinu za kimapambano na kuilinda nchi kwa uzalendo. Hapa kijana akimaliza hutoka bila cheo na hutumika ktk division aliyopangiwa either infantry, anga, navy n.k!

Enzi za nyuma wengine waliingia JW kwa vipaji vyao na kupata vyeo vikubwa mf Captain Komba alijoin due to kipaji cha kuimba (I stand to be corrected)

Please, kuna anayeweza kunipanulia uelewa kdg ni vigezo vp hutumika kumchagua mtu akasomee staff cardet? Je, ni criteria gani huzingatiwa ili kijana aende further courses mpaka ukomandoo?

Je, wanawake huweza kufikia level ya komandoo hasa hapa Tz?

NB: wanachuo, zile swaga za ooh, ukiwa na degree unafikia sijui nyota moja jeshini futeni. Kule unastart afresh unless umeajiliwa as professional. Stop cheating one another! Vyeo sio karanga au njugu mnazogawiana kwenye kahawa!

Just for learning!
Karibu.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwa kuanzia tu hakuna kozi kama hiyo katika JWTZ labda kama ulikuwa unamaanisha Officer Cadet.
Hicho ndiyo cheo cha kwanza kabisa katika Jeshi lolote ikiwa ni pamoja na JWTZ letu ila ni cheo anachopewa mwanafunzi wa ngazi ya uafisa ambacho ni cha juu kuliko vyeo vyote visivyo vya kamisheni. Jeshi lina aina mbili za vyeo; visivyo vya kamisheni, yaani Non Commissioned Officers (NCO) na Commissioned Officers. Mwenye ngazi hiyo yuko juu ya vyeo vyote vya maaskari ila anakosa mamlaka hadi anapotunukiwa "Kamisheni" ambayo kwa kawaida hutolewa na Mkuu wa nchi husika kama Rais, Mfalme, Malkia au Waziri Mkuu kwa nchi ambazo Mkuu wa nchi ni Waziri Mkuu.
Utaratibu wa kuwapata Ma Officer Cadets ni wa kawaida yaani huteuliwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi husika zikiwemo uchunguzi kuhusiana na tabia njema isiyo shaka, uwezo wa kutafakari na kufikiri na mara nyingine kuna mitihani maalum kwa zoezi hilo. Wateule hawa hupekwa kwenye vyuo maalum vya kijeshi vyenye hadhi fulani, kupitia mafunzo magumu yenye kuwapima uvumilivu, ujasiri, uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi sahihi, usafi na vigezo vingi sana ambapo wanaobainika kushindwa hurudishwa na wanaofaulu kutunukiwa uofisa; ndiyo Kamisheni - cheo cha kwanza kwa maofisa lakini chenye hadhi kubwa kabisa; kwani kwa kutunukiwa cheo hicho Afisa huwa na hadhi sawa na Afisa yeyote Jeshini wakitofautiana vyeo, madaraka na nafasi. Afisa wa cheo hiki anaweza kupandishwa kwenye nafasi yoyote ya ki Afisa litokeapo hitaji.
 
Uko sahihi, kwa kuongezea chuo cha maafsa ni kimoja nchi nzima ili kumaintain discipline na standards,, ndo
Maana Uk wana sandhurst, marekani wana west point, hyo kozi unayoita staff cadet haipo duniani
 
Kwa kuongezea ukomandoo sio cheo jeshini ni fani moja wapo kati ya nyingi zilizopo huko.
 
Back
Top Bottom