BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
Salamu Waungwana. Nina kijana wangu amemaliza F4 mwaka jana lakini kwa bahati mbaya alipata Dv 4 ya pointi 30. Nipo kwenye mikakati ya kumhangaikia. Nimesikia kuwa hapo UDSM huwa kuna kozi za mwaka mmoja mmoja za Certificate ambazo hata waliomaliza F4 wanaweza kujiunga nazo kutegemea na kozi husika na alama alizopata mwanafunzi kwenye mtihani wa F4.. Naomba kwa mwenye ufahamu nazo anijulishe/atujulishe hapa ni kozi aina gani zinazotolewa/muda gani/ada yake na mambo kama hayo. Natanguliza shukurani.