Kozi za Certificate Mlimani

Kozi za Certificate Mlimani

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Posts
6,122
Reaction score
4,060
Salamu Waungwana. Nina kijana wangu amemaliza F4 mwaka jana lakini kwa bahati mbaya alipata Dv 4 ya pointi 30. Nipo kwenye mikakati ya kumhangaikia. Nimesikia kuwa hapo UDSM huwa kuna kozi za mwaka mmoja mmoja za Certificate ambazo hata waliomaliza F4 wanaweza kujiunga nazo kutegemea na kozi husika na alama alizopata mwanafunzi kwenye mtihani wa F4.. Naomba kwa mwenye ufahamu nazo anijulishe/atujulishe hapa ni kozi aina gani zinazotolewa/muda gani/ada yake na mambo kama hayo. Natanguliza shukurani.
 
labda computer kozi ndo haina masharti magumu, Kwa four ulioisema, certificate ya sheria na tour guild asiguse kabisa maana viwango vya kuingilia ni vya juu na ushindani ni mkubwa
 
sua kuna certificate ya IT,jaribu huko ila sijui wanaingia na four ya ngap,pia SAUT mwanza wana course kibao za certificate sio lazima asome mlimani elimu popote ilimradi apaete content zitakazomweka kwenye ushindani wa ajira
 
mpeleke vyuo vya ilala na kariakoo kwa matokeo yake ndio itakuwa rahisi kupata, hapa mlimani ushindani ni mkubwa sana.
 
mpeleke vyuo vya ilala na kariakoo kwa matokeo yake ndio itakuwa rahisi kupata, hapa mlimani ushindani ni mkubwa sana.
 
Ninawashukuru nyote kwa information hizi muhimu. Kwa ujumla ni kwamba course za certificate ila ushindani ndio unakuwa mgumu sana. itabidi akashindane. kwa mujibu wa brosure ziko kozi nyingine zaidi ya hizo 2 za law na IT. Hara hivyo naona tumeishachelewa maana brosure yao inasema mwisho wa maombi ilikuwa ni tar 30 June na masomo yanaanza katikati ya Julai na ada ni 1,430,000/=
 
mpeleke vyuo vya ilala na kariakoo kwa matokeo yake ndio itakuwa rahisi kupata, hapa mlimani ushindani ni mkubwa sana.
...Nakubaliana nawe mkuu sema sasa huko mbele wakati wa kusaka ajira mwenzake akimwaga cheti cha UDSM Computing Center na yay akamwaga cha 'Chaurembo Kompyutingi Senta' cha Buguruni Malapa. otea nani atapata ajira...!!
 
Mpeleke pale TLSB akasome kozi za library anze na elementary level then atakuwa ameongeza sifa atajiunga na certificate level atafika mbali sn.
 
Salamu Waungwana. Nina kijana wangu amemaliza F4 mwaka jana lakini kwa bahati mbaya alipata Dv 4 ya pointi 30. Nipo kwenye mikakati ya kumhangaikia. Nimesikia kuwa hapo UDSM huwa kuna kozi za mwaka mmoja mmoja za Certificate ambazo hata waliomaliza F4 wanaweza kujiunga nazo kutegemea na kozi husika na alama alizopata mwanafunzi kwenye mtihani wa F4.. Naomba kwa mwenye ufahamu nazo anijulishe/atujulishe hapa ni kozi aina gani zinazotolewa/muda gani/ada yake na mambo kama hayo. Natanguliza shukurani.
mkuuu nimesoma post yako ila mimi nakushauli kitu kimoja muulize anapenda kuwa nani na mtafutie kozi nzuli yenye uhakika na ajira sokoni......anaweza pata mshahara mzuli kusoma udsm sio inshu wala nini....maana kufanikiwa siku hizi ni popote ila mi ushauli wangu mtafutie kozi yenye uhakika
 
Nakushauri uende pale Mlwimu Nyerere Mlimani Campus moja kwa moja UCC uwaone watakusaidia sana. Kama uko mkoani utawakuta Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma. Jaribu ukose kuliko kuacha au kukatishwa tamaa baadaye uakjutia
 
Mkuu C Programming nimekupata. Kijana ameniambia luwa angependa sana kwenye mambo ya uwakili nk kwa maana hiyo yuko tayari kuanzia kwenye certificate ya Law. Alitaja pia Records Management ambayo watu wengi wanaitaja sana siku hizi ingawaje mimi sijakuwa convinced sana na ajira yake na kwamba unaweza kufika wapi nayo. Mkuu Mabulangati, ushauri wako ni mwema na nitautekeleza na kuja kutoa feedback. Pia option ya TLSB kama alivyochangia Kapistrano ni mwema na ninaweza kuuchukua kama Plan B iwapo huku kote kuta-fail. Mbarikiwe sana Wakuu. .
 
Ninawashukuru nyote kwa information hizi muhimu. Kwa ujumla ni kwamba course za certificate ila ushindani ndio unakuwa mgumu sana. itabidi akashindane. kwa mujibu wa brosure ziko kozi nyingine zaidi ya hizo 2 za law na IT. Hara hivyo naona tumeishachelewa maana brosure yao inasema mwisho wa maombi ilikuwa ni tar 30 June na masomo yanaanza katikati ya Julai na ada ni 1,430,000/=

mpelekeTIA wanakozi nyingi za certificate kama vile accounting na procurement.SAUT wanaanzisha certificate ya Librarian and records management. tawi la mtwara wanaanza mwaka huu. wanataka minimum D 4 tu. kwa huyo anapata. kwa TIA ada ni laki 7 na SAUT ni laki 8 na nusu. tembelea tovuti at ofisi za any of the 2 colleges.
regards.
 
mkuu pia jaribu pia vyuo vya UHAZILI vilivyopo TABORA,MTWARA na DAR-ES-SALAAM wao certificate uwe na D nne na kuendelea
 
Mkuu C Programming nimekupata. Kijana ameniambia luwa angependa sana kwenye mambo ya uwakili nk kwa maana hiyo yuko tayari kuanzia kwenye certificate ya Law. Alitaja pia Records Management ambayo watu wengi wanaitaja sana siku hizi ingawaje mimi sijakuwa convinced sana na ajira yake na kwamba unaweza kufika wapi nayo. Mkuu Mabulangati, ushauri wako ni mwema na nitautekeleza na kuja kutoa feedback. Pia option ya TLSB kama alivyochangia Kapistrano ni mwema na ninaweza kuuchukua kama Plan B iwapo huku kote kuta-fail. Mbarikiwe sana Wakuu. .

Kuna chuo cha uhakimu pia Lushoto, zamani walikuwa wanatoa certificate, sijui siku hizi
Chuo cha Horombo kitafaa sana katika masuala ya records management
 
Mkuu nakubaliana na ushaur wa C Programming siku hizi watu hawaangalii ulikosoma huwa wanaangalia ufahamu wako wa mambo ila kwa kuwa dogo anataka mambo ya law unaweza kwenda hapo UCC Mliman Campus hata kama deadline imeshapita labda wanaweza kukusadia,kwa mtazamo wangu naona Record Managements haifai coz kuna utitiri wa wanafunz wengi wanaoisomea lakin pia uhakika wa ajira hamna tofauti na Law.
 
Mkuu nakubaliana na ushaur wa C Programming siku hizi watu hawaangalii ulikosoma huwa wanaangalia ufahamu wako wa mambo ila kwa kuwa dogo anataka mambo ya law unaweza kwenda hapo UCC Mliman Campus hata kama deadline imeshapita labda wanaweza kukusadia,kwa mtazamo wangu naona Records Management haifai coz kuna utitiri wa wanafunz wengi wanaoisomea lakin pia uhakika wa ajira hamna tofauti na Law.
 
Jamani na mtu aliyesoma EGM anaweza somea Computer science chuo kikuu gani!
 
Back
Top Bottom