...Nakubaliana nawe mkuu sema sasa huko mbele wakati wa kusaka ajira mwenzake akimwaga cheti cha UDSM Computing Center na yay akamwaga cha 'Chaurembo Kompyutingi Senta' cha Buguruni Malapa. otea nani atapata ajira...!!mpeleke vyuo vya ilala na kariakoo kwa matokeo yake ndio itakuwa rahisi kupata, hapa mlimani ushindani ni mkubwa sana.
mkuuu nimesoma post yako ila mimi nakushauli kitu kimoja muulize anapenda kuwa nani na mtafutie kozi nzuli yenye uhakika na ajira sokoni......anaweza pata mshahara mzuli kusoma udsm sio inshu wala nini....maana kufanikiwa siku hizi ni popote ila mi ushauli wangu mtafutie kozi yenye uhakikaSalamu Waungwana. Nina kijana wangu amemaliza F4 mwaka jana lakini kwa bahati mbaya alipata Dv 4 ya pointi 30. Nipo kwenye mikakati ya kumhangaikia. Nimesikia kuwa hapo UDSM huwa kuna kozi za mwaka mmoja mmoja za Certificate ambazo hata waliomaliza F4 wanaweza kujiunga nazo kutegemea na kozi husika na alama alizopata mwanafunzi kwenye mtihani wa F4.. Naomba kwa mwenye ufahamu nazo anijulishe/atujulishe hapa ni kozi aina gani zinazotolewa/muda gani/ada yake na mambo kama hayo. Natanguliza shukurani.
Ninawashukuru nyote kwa information hizi muhimu. Kwa ujumla ni kwamba course za certificate ila ushindani ndio unakuwa mgumu sana. itabidi akashindane. kwa mujibu wa brosure ziko kozi nyingine zaidi ya hizo 2 za law na IT. Hara hivyo naona tumeishachelewa maana brosure yao inasema mwisho wa maombi ilikuwa ni tar 30 June na masomo yanaanza katikati ya Julai na ada ni 1,430,000/=
Mkuu C Programming nimekupata. Kijana ameniambia luwa angependa sana kwenye mambo ya uwakili nk kwa maana hiyo yuko tayari kuanzia kwenye certificate ya Law. Alitaja pia Records Management ambayo watu wengi wanaitaja sana siku hizi ingawaje mimi sijakuwa convinced sana na ajira yake na kwamba unaweza kufika wapi nayo. Mkuu Mabulangati, ushauri wako ni mwema na nitautekeleza na kuja kutoa feedback. Pia option ya TLSB kama alivyochangia Kapistrano ni mwema na ninaweza kuuchukua kama Plan B iwapo huku kote kuta-fail. Mbarikiwe sana Wakuu. .