Kozi za urubani Tanzania zina gharama gani?

Joined
Jan 30, 2015
Posts
6
Reaction score
4
Naomba mwenye ufahamu wa gharama za kozi ya urubani zinazotolewa pale United Tanzania Aeronautics College (www.utac.ac.tz) - Airport Dar es salaam .

Katika matangazo yaliyo kwenye website hawajaainisha gharama za masomo hayo.Pia je kuna vipindi vya jioni yaani evining classes, ili nikachukue form Tsh 50,000 mara moja kabla sijachelewa. Mwenye kufahamu naomba anijulishe.
 
daaaaah kumbe kuna kozi za urubani hapa Tz, ndo nmesikia leo.
 
Kozi za urubani zipo hv. Kuna PPL(PRIVATE PILOT LICENCE), hii unasomea leseni ya kuendesha ndege za private, hii haina dili sana ila ndo ya kuanzia. Kwa hiyo pale Tropical air walikuwa wanatoza dollar 17000.

CPL(COMMERCIAL PILOT LICENCE), hii ndo yenye dili, ni leseni ya kibiashara, yani kama class C kwenye magari, wengi wanasomea South Africa baada ya kupata PPL, andaa milioni 50.

Kazi kwako kaka. Huu ndo ufahamu wangu
 

aksante ndugu kwa kunielimisha
 
Kuna jamaa angau pale osterbay alienda kusomea uruban canada kardi bong anaishia kpga dayworker tu za kwenda mbugan na kuvaa nguo za babke kuzngka nazo mtaan eti ajulkane ni captain teh teh teh
wish u all the best mkuu
 

Mamama mae... Ukiwa na Pesa kama hizo usome ili upate nini???? Wakati unaambiwa Bongo hupati kazi hata kama Umesoma... na Ukijapata basi utapewa kazi za Data Entry.... mamama mae...

Pesa kama hizo nanunua Ubunge... nikaishi zangu Idodomya...
 
Mimi nitasomea just for fun maana nilikuwa napenda hii kitu sana toka class five hadi form six
 
tafuta vyuo vya south africa ukimaliza utapata madili hukuhuko bongo mizinguo tu
 
kama wenzangu walivyokwisha kueleza hapo awali kiukweli kozi zao gharama zao ni ghali mno. nina rafiki yangu amesomea mambo ya information technology ila anataka sana kusomea urubani. sasa kutokana na cost nikamwambia ajaribu kucheki kama atapata chuo nairobi. ila akaniambia kuwa amesikia NIT chuo cha usafirishaji kilichopo pale mabibo kikombioni kuanza kufundisha hiyo kozi pale. ila ndg kama unavyojua tanzania yetu tunaongea sana ila vitendo ni zero, kwani unaweza kusubiri hapo NIT na usione kitu. jaribu kucheki S.A kama mkuu alivyokushauri hapo juu. kila la kheri
 
Ndugu usiogope cost katka jambo ambalo unatamani kulipata,zamani nilitamani kuwa rubani tena sana ila baada ya kuona ndugu zangu wanakufa kwa huu ugonjwa wa kisasa nikaamua kusomea udaktari,gharama ilikuwa kubwa mno na bahati mbaya au nzuri nilipata chuo india so ilibdi kujifunga mkanda ili niweze kutmiza ndoto yangu,leo hii mimi ni mtu ambae nayafurahia maisha,nimejiajiri na sina ndoto ya kuajiriwa.

Hivyo na wewe usikate tamaa kwa vile nia ipo moyoni mwako utafanikiwa tu,jambo muhimu kuwa makini kuchagua marafiki maana ukiwa na marafiki ambao hawaangalii mbele watakukatsha tamaa kuwa na rafiki ambao wanaamini kuwa "INAWEZEKANA" ambao wanatamani kuyaona mafanikio yako.
 
ok,
na kozi hizi zinazotolewa na Tanzania Aviation University College www.tauc.ac.tz Tabata Magengeni, zinatolewa gharama gani. Mwenye ufahamu naomba anisaidie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…