Kaka upo nje kabisa ya mada, wewe ndiye unayezungumza siasa, TRA ipo na matatizo ya kiutendaji kama ilivyo KRA.
Kawaida huwezi kulinganisha makusanyo ya nchi mbili zenye uchumi tofauti kwa kuangalia kiwango kilichokusanywa, badala yake unaangalia ni asilimia ngapi ya GDP ya hiyo nchi imewezwa kukusanywa, hapo ndio unaweza kupima ufanisi wa makusanyo ya kodi.
Kawaida nchi inapaswa kukusa 24% ya GDP yake kama kodi, Kama nchi ikifanikiwa kukusanya 24% ya GDP, hiyo ndio 100% ya ukusanyaji kodi, lakini hakuna nchi ambayo imeshafikia huko, nchi nyingi zinazofanya vizuri zipo kati ya 18 to 21%.
Kwa mara ya mwisho data za BoT zilionyesha Tanzania tunakusanya 15% na Kenya 16 %(sikumbuki vizuri). Kwahiyo hatupaswi kulinganisha kiwango badala yake tulinganishe % ya ukusanyaji wa mapato