Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Klabu ya KRC Genk imetwaa rasmi ubingwa wa ligi kuu ya soka ya nchini Ubelgiji, Belgium Jupiler League kwa msimu wa kuanzia 2018/2019.
Klabu hiyo ya KRC Genk ambayo anakipiga nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambaye pia ni kinara wa mabao kwenye ligi hiyo ya Ubelgiji, Mbwana Samatta Samagoal77, imetwaa ubingwa baada ya kutoka sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Anderlecht na kuweza kufikisha pointi 51 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.
Ubingwa huo wa KRC Genk umepatikana baada ya wapinzani wao wa karibu kwenye kinyang'anyiro Uchampioni, Club Brugge kupoteza mchezo wao kwa kipigo cha mabao 2-0 mbele ya Standard Liege hivyo kupoteza uwezo wa kufikisha pointi 51 huku ukiwa umebaki mchezo mmoja katika mchuano wa timu sita bora.
Kwa ubingwa huo KRC Genk wamepata nafasi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.