Krismas ya mwaka huu yawa ya mfano, Chadema wahaha

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Shamrashamra za sikukuu ya krismas mwaka huu 2018 zimekuwa za mfano na kuwaacha Chadema mdomo wazi.

Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao walikuwa wamejiandaa kutumia sikukuu za mwisho wa mwaka huu kuwaeleza na kuwaonyesha wananchi na dunia kwa ujumla jinsi vyuma vilivyokaza hapa Tanzania! Lakini hali imekuwa tofauti na matarajio ya CHADEMA. Sokoni watu wamejaa, kwenye bar watu wamejaa, kwenye mabasi watu wamejaa hadi hayatoshi kuwasafirisha!. Nyama inanunulika kwa sana na mialiko ni ya kutosha!

Hali hii imewaacha CHADEMA katika hali mbaya mno kisiasa na wanatafakari waje na gia ipi nyingine baada ya hii ya vyuma kukaza kubuma.
 
Kweli hata jela watu wa mejaa hospitalini watu wamejaa msibani watu wamejaa, big up CCM.
 

 
Wananchi wanaChadema wenyewe wapo busy. Wengi wanatokea kaskazini. Huku hata vyuma vikaze vipi hayo uliyoyataja yatafanyika. Watu wa kaskazini wanajua kuweka reserve ya miaka kibao mbele. Na hii nchi ingekuwa kila Kanda inajijenga yenyewe halafu kuwe kuna mchango kwa serikali kuu kwa ajili ya nchi' ndo ungeielewa kaskazini. Ni vile utaratibu wetu ni wa kukusanya zote kwenye bakuli moja.
 
Misifa ya kijinga hii, jiji la kwanza maendeleo ni Dar kwa wazaramo na jiji la pili kwa maendeleo ni Mwanza kwa wasukuma
 
Aisee ungejua hata usingeleta hii mada... kwa nini mnapenda uongo...


Cc: mahondaw
 
Reactions: BAK
Sasa mlipe kodi
 
Misifa ya kijinga hii, jiji la kwanza maendeleo ni Dar kwa wazaramo na jiji la pili kwa maendeleo ni Mwanza kwa wasukuma
Hayo madaraja, bandari na mambo mengine kibao unadhani yamejengwa kwa kutumia kodi zinazokusanywa kutoka kwa wazaramo? Kaskazini kuna utalii, madini, ufugaji na kilimo. Nenda kaangalie mchango wa hizi sekta kwa serikali. Na hilo jiji wala wazaramo hawalitendei haki' wafanya biashara wengi wametoka mbali.
 
Nawahurumia walio pata tabu ya kukuleta hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…