Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Msemaji wa Mbezi Beach nimekuja kwa mara nyingine.
Kwa Mbezi maji yanakatika kila siku na wakati mwingine inaweza kuwa siku mbili na zaidi. Muda wa kukatika ni kuanzia jioni (kwenye saa kumi hivi) mpaka kesho yake kwenye saa nne au tano hivi. Kwahiyo kwa siku mara mnyingi maji hutoka kama masaa 6 hivi.
Najua mtauliza kuhusu matenki na kuhifadhi maji. Wengi tuna matenki ya kuhifadhia maji lakini asilimia 98 maji hutoka kwa presha ndogo kwahiyo hata kama una tenki bado ni useless! Siku hiyo tumemulikwa na tochi ka presha kakaongezeka ukasahau kufungua tenki ndio imetoka hiyo, kuja kuipata presha hiyo ni kwa bahati sana.
Krismasi maji yaliyoka bila tabu, na presha ilikuwa nzuri, ila baada ya hapo tumerudi kwenye mgao!
Sasa hii inamaanisha nini Wizara ya Maji?
1. Mnafanya makusudi kutukatia maji ili watu wafanye biashara
Nilikua sijaona siku nyingi watu wakifanya biashara ya maji kwenye madumu na wanawake kuhangaika kuchota maji, hili sasa ni kawaida!
2. Ni hujuma, watendaji wanakuangusha Waziri Wizara ya Maji
Ulijitapa kuwa Mbezi Beach ni moja ya maeneo ambayo yana huduma bora ya maji, kitu ambacho ni uongo sababu tunapata joto la jiwe utafikiri ni kitu tunaomba! Hivyo inawezekana kweli huduma ni nzuri lakini kuna watu wanahujumu ili mufanya biashara zao.
3. Waziri Aweso Wizara ya Maji najua kwamba huduma ni mbovu ila umeamua kutufanya wote wajinga kwa maslahi yako binafsi, huenda ni mmoja wa wafanyabiashara wanaokwamisha huduma hii
Unajua kinachoendelea ila unatuigizia na kuendelea kupiga zako pesa, kutwa kuigiza na mapicha picha kwenye mitandao ili uonekane unafanya kazi na kutupa majibu kisiasa wakati wewe ndio mkwamishaji wa kwanza wa huduma hii, na kwakuwa una ka imani ka Rais basi unajiona we ndio wewe tena, mfalme wa maji, wa kuamua nani apate nani umkomeshe, na unatukomesha kweli
4. Kuna upungufu mkubwa wa maji unaosababisha mgao na hamtaki kuujulisha sababu unajua kuna maswali magumu yatakuja na huna majibu yake, na hii itapelekea wewe kutumbuliwa.
Mvua ilinyesha ya kutosha, maji yakavunwa ya kutosha tukaaminishwa kuwa hatutakuwa na mgao, halafu ghafla tuna mgao. Kuna kitu kimefanyika huko mpaka tumepoteza maji. Kusema hili kwa umma ni msala si tu kwa wananchi bali hata kwa bosi wako anayetegemea mfanye kazi nzuri ili ajihakikishie ushindi 2025. Na hili mimi ndio naona kinachotokea sasa hivi.
Ambapo kuliko kuficha watu tunahangaika kila siku na kupata huduma ambayo hairidhishi bora tuambiwe ukweli, ratiba itoke, tujue kwa wiki tunapata maji siku tatu, au nne, yakitoka yanatoka kwa presha kubwa tunaweza kuhifashi kuliko ilivyo sasa, hata kama yanatoka ni useless, ya kutumia hapo hapo labda na kuweka kwenye ndoo mbili tatu!
Mnafanya mpaka watu wanataka Makonda apewe wizara ya maji ili awanyooshe, maana yeye anaonyesha kwa vitendo, mbali na u psycho wake, walau anadeliva!
Pangani wakichagua 'bumunda' wewe mwakani tutawaroga wote😩😩😩, Aweso Wizara ya Maji ni moja ya upotevu wa kodi zetu kipuuzi kabisa, bomu!
Sina maji hata tone halafu uko bize kujionesha mtandaoni, njoo mtaani hutaki, njoo kwenye group uone uhalisia hutaki. Huyo Rais 'akurambe' tu urudi pangani kulima kungu, labda tutapata huduma bora mtu mwingine akishika nafasi hiyo!