neno ni upanga
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 494
- 1,656
SOMO: SIKUKUU YA CHRISTMASS NI MAPOKEO YA WANADAMU WALA SIO MAAGIZO YA MUNGU
Wakolosai 2:8
Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
Katika maisha ya wokovu ambao tunaishi, Mungu ametupa neno lake lituongoze na kutukamilisha tunapolisoma kila iitwapo leo na kujifunza maana ya hilo neno
Wakolosai 3:16
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Hivyo sisi ambao ni watu ambao tunatumia biblia lazima kila tulifanyao Liwe na rejea kwenye maandiko
Zekaria 3:7
BWANA wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Ukisoma biblia yote kuanzia mathayo mpaka ufunuo hamna sehemu walisherekea au kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu tofauti na sherehe zingine kama pasaka au kufa na kufufuka kwa Yesu,
Hata Yesu baada ya kuzaliwa ameishi duniani miaka 33, lakini hiyo miaka yote hamna sehemu ilipoandikwa kuwa walimfanyia sherehe ya siku kuu ya kuzaliwa kwake! Tunachokifanya watu tuliokoka tumerithi mapokeo ya wanadamu
Marko 7:8
Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
Marko 7:9
Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
Mitume nao pamoja na kuhubiri kwao, na kutoa nyaraka mbalimbali hamna sehemu walisherekea kuzaliwa kwa Yesu, au kulikumbusha kanisa kwenye nyaraka zao kuhusu kusheherekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu
2 Timotheo 2:2
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
Biblia imeeleza wazi kuwa tutahukumiwa sawasawa na injili ya paul kwa Kristo Yesu, swali linakuja kama mitume pamoja na paul mwenyewe hawakusherehekea sikukuu hii je sisi tunasherekea kwa Kibali cha nani?????
Warumi 2:16
katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Maanake tunasheherekea CHRISTMASS kwa Kibali cha mafundisho au maagizo ya wanadamu
Wakolosai 2:22
(mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?
KWA NINI SIKU KUU YA KUZALIWA KWA YESU HAIKUADHIMISHWA KWENYE BIBLIA
1: kibiblia siku ya kuzaliwa haipewi kipao mbele sana kwa sababu ni siku ambao mwanadamu anakuja kwenye dunia iliyojaa dhambi, hivyo kibiblia walioisherekea walisherehekea kwa mafunuo yao wala sio ya KiMungu,
Tito 3:5
si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
biblia imeipa hadhi kubwa siku ya kuzaliwa kiroho yaani siku mtu anapookoka ndo siku yenye furaha mpaka mbinguni
Yohana 1:12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Yohana 1:13
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
2: kusherekea Siku ya kuzaliwa kibiblia inachukuliwa kama ni sehemu ya kufanya anasa, hata wote waliosherehekea waliotajwa walifanya matukio ya anasa, mpaka wengine siku hii walimkosea Mungu sana, rejea kwa herode nk
Mathayo 14:6
Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
Mwanzo 40:20
Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
Ukiangalia waliosherehekea siku zao kibiblia ni watu ambao hawamjui Mungu, na hata sherehe hizo hazikuwa na utukufu mbele za Mungu
3: hamna mtakatifu yeyote kwenye biblia aliyesherehekea Siku yake ya kuzaliwa, tukianzia kwa baba wa imani ibrahimu, isaka, yakobo, musa, Ayubu, daudi, mitume wa Yesu nk, wote waliosherekea siku yao ya kuzaliwa ni wapagani tu, je sisi tuliokoka tumejifunza kwa nani??? Tunaposherekea siku ya kuzaliwa kwetu pamoja na christmass????
Wafilipi 4:9
Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
Lazima watu tuliokoka kila tunalolifanya tuwe na reference tumejifunza kwa nani, kwa Yesu, kwa paul, mitume na manabii au tumejifunza kwa farao na herode?????
2 Timotheo 3:14
Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;
Kanisa la Mungu limejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na hao manabii na mitume wa Mungu hamna mtu hata mmoja alisherehekea siku yake ya kuzaliwa je! Wewe mkristo umejifunza kwa nani????
Waefeso 2:20
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
JE KUSHEREHEKEA CHRISTMASS NI KOSA
jibu hapa ni ndiyo ni makosa kwa sababu sio maagizo ya Mungu,
Mathayo 15:9
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Hii tarehe 25 /12 kila mwaka ilikuwa sikukuu ya kipagani, hivyo sisi tuliokoka tunaruhusiwa kutumia sikukuu ya kipagani tukasherekea pamoja????? Jibu hapana
2 Wakorintho 6:16
Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Hii Siku uchafu mwingi hufanyika kwa sababu haimbatani na utakatifu wa Mungu ndani yake, ni siku ambayo inawaingiza watu kwenye madeni, imejaa anasa za kila aina hivyo mbele za Mungu hataki hata kusikia makelele yenu
Amosi 5:21
Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.
Amosi 5:22
Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.
Amosi 5:23
Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.
Hivyo mpendwa wewe uliyeokoka wasabato kwenye hili wameokoka, sisi tuliokoka kusheherekea Christmass sio sahihi na sio sahihi, na sio sahihi najua wengi watapinga lakini wapo watakalolipokea neno hili
Mathayo 19:11
Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
Mungu atusaidie kuijua kweli ya maandiko,