Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Leo ni sikukuu ya Christmas .. Siku kubwa ulimwengu kote.. Kwa wiki nzima hii yametokea matukio ambayo yatakuwa ni simulizi za kukumbuka miaka mingi iijayo
Mimi ninazo simulizi mbili nawe kama unayo uta share nasi
Ukata Christmas ya 1993
ilikuwa kipindi cha Mwinyi
Tumeshamaliza chuo tulitakiwa kwenda jeshini kisha ajira.. Serikali ikawa haina hela za kutupeleka jeshini wala kutupa ajira.. Ule msoto ule wee acha tu
Ikawa sasa ni mwendo wa vibarua... Na kutembelea fursa..wakati fursa kubwa kipindi cha Christmas ukiachana na vyakula toka mikoani ni miti ya Christmas
Sasa hii kwetu ipo mingi sana hivyo unakata tu bila kulipa chochote
Nikapanga na jamaa yangu yeye huko mkoani akate akodi fuso apakie mimi nitapokea mzigo Ubungo palipokuwa kituo kikuu cha uuzaji
Timing ya miti ya Chtistmas ilikuwa ni siku nne za mwisho kabla ya sikukuu yenyewe
Logistics na kukata na kupakia zikatuchelewesha kwa siku moja nzima!
Fuso likaingia Ubungo tarehe 24 mchana... Pakiwa pamefurika miti😂 tena mizuri kuliko yetu
Hatukuweza kuuza hata miti kumi kati ya miti zaidi ya 150 tuliyobeba
Fuso hatukuwa tumelipia hata senti.. Tuliukimbia ule mzigo tukamtelekeza dereva na konda wake pale Ubungo Tanesco
Uzuri hakukuwa na simu za mkononi.. Walimiliki wachache tena matajiri
Kwetu sisi siku kama ya leo tarehe 25.12.1993 ilikuwa siku mbaya ya kukumbukwa daima
Mwisho wa simulizi ya kwanza