Krismasi za kukumbuka (sad memories)

Krismasi za kukumbuka (sad memories)

1993-2024=31
Ilikufanya hayo uliyosema si chini ya umri wa miaka 20!

Mara nyingi hizi zinakuwa ni hadithi za kuhadithiwa au hualisia wake ni mdogo sana .
Tatizo lenu mnadhani watu wote humu JF ni vijana wadogo. Tumo Babu, Bibi, Baba na Mama zenu humu.
 
Hii imekaa kama kamba, mwaka 2000 simu ya mkononi na gesi ya kupikia?!!
Gas ya kupikia ipo muda mrefu sana. Sisi tumeitumia nyumbani miaka ya mwisho ya 1970s hadi leo natumia. Simu ya mkononi kwa mara ya kwanza nimeitumia mwaka 1994 na haikuwa ya kwangu!! Nilimiliki simu ya mkononi kwa mara ya kwanza mwaka 1998 ilikuwa Motorola. Niliitunza ili niwaonyeshe wajukuu zangu bahati mbaya watoto wangu waliitupa.
 
Mbona hizo stori zenu za miaka wengine bado hatujazaliwa🤕
Ndiyo ufahamu humu tumo Babu, Bibi, Baba na Mama zenu!!! Kuna baadhi ya watu humu huwa wanajibu watu vibaya kama vile wote tuliomo humu tuna umri unaolingana na tumezaliwa kuanzia miaka ya 1995!!!!
 
Sasa ndonaelewa wazazi walikua wanapitia presha ya kiwango kipi pale sikukuu zinapokuja na ela hakuna nyumbani,tulikua tunajiliza tukikosa nguo za sikukuu ila sasa ndonaelewa wanangu wanaponigizama sikukuu imefika na sina ela
Mimi niliwazoeza watoto wangu tangu wakiwa wadogo kuwa nitawanunulia nguo pale wanapohitaji na siyo kila siku kuu ya Christmas na Pasaka. Wakakua wanaelewa hivyo, sikuwahi kupata pressure hizo.
 
Umepitia mengi sana kwenye maisha, na kwa story zako inaonekana ni mkubwa wangu, mwaka ambao upo chuo mimi bado nilikuwa dereva wa sinia kwa wazazi
Umri umeenda sasa.. Nakaribia kurudisha mpira kwa kipa😭
Chrismass ya Mwaka 1989 ilinikuta na pacha wangu vibaya sana. Tulikuwa tumemaliza Darasa la SABA na matokeo ni kuwa HATUKUCHAGULIWA kwenda sekondari.

Niliona ndo mwisho wa maisha maana kukosa kwenda seko ilikuwa ni kama Huna future tena. Hatukuwa na furaha kabisa na sikukuu haikuwa na maana tena.
Mwaka huo Nilikuwa form one! Log jua linakuchwa sasa😭😭😭
 
Gas ya kupikia ipo muda mrefu sana. Sisi tumeitumia nyumbani miaka ya mwisho ya 1970s hadi leo natumia. Simu ya mkononi kwa mara ya kwanza nimeitumia mwaka 1994 na haikuwa ya kwangu!! Nilimiliki simu ya mkononi kwa mara ya kwanza mwaka 1998 ilikuwa Motorola. Niliitunza ili niwaonyeshe wajukuu zangu bahati mbaya watoto wangu waliitupa.
Umenikumbusha Sony Savy simu mbovu sijapata kuona😭😂
 
Hata majina sikumbuki sahiv, ila alikuwa anaishi karibu na posta (zamani) pale round about (tulikuwa tunaita mwenge wa bandia) mbele kidogo. Sijui kama sahivi kuna mazingira hayo. Maana sasa yapata zaid ya miaka 25
Panaitwa Upogoroni, kuna Wapogoro wengi maeneo hayo chakula chao Ngalange
 
Back
Top Bottom