Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Huu muda NECTA wanapenda kutoa matokeo, wanakuamulia Christmas njema au mizozo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ikabidi ujikatae fasta kabla akijanuka aisee maisha aya sio powaLeo ni sikukuu ya Christmas .. Siku kubwa ulimwengu kote.. Kwa wiki nzima hii yametokea matukio ambayo yatakuwa ni simulizi za kukumbuka miaka mingi iijayo
Mimi ninazo simulizi mbili nawe kama unayo uta share nasi
Ukata Christmas ya 1993
ilikuwa kipindi cha Mwinyi
Tumeshamaliza chuo tulitakiwa kwenda jeshini kisha ajira.. Serikali ikawa haina hela za kutupeleka jeshini wala kutupa ajira.. Ule msoto ule wee acha tu
Ikawa sasa ni mwendo wa vibarua... Na kutembelea fursa..wakati fursa kubwa kipindi cha Christmas ukiachana na vyakula toka mikoani ni miti ya Christmas
Sasa hii kwetu ipo mingi sana hivyo unakata tu bila kulipa chochote
Nikapanga na jamaa yangu yeye huko mkoani akate akodi fuso apakie mimi nitapokea mzigo Ubungo palipokuwa kituo kikuu cha uuzaji
Timing ya miti ya Chtistmas ilikuwa ni siku nne za mwisho kabla ya sikukuu yenyewe
Logistics na kukata na kupakia zikatuchelewesha kwa siku moja nzima!
Fuso likaingia Ubungo tarehe 24 mchana... Pakiwa pamefurika miti😂 tena mizuri kuliko yetu
Hatukuweza kuuza hata miti kumi kati ya miti zaidi ya 150 tuliyobeba
Fuso hatukuwa tumelipia hata senti.. Tuliukimbia ule mzigo tukamtelekeza dereva na konda wake pale Ubungo Tanesco
Uzuri hakukuwa na simu za mkononi.. Walimiliki wachache tena matajiri
Kwetu sisi siku kama ya leo tarehe 25.12.1993 ilikuwa siku mbaya ya kukumbukwa daima
Mwisho wa simulizi ya kwanza
Bibi yako anakaa sehemu gani? Hapo ifoza mimi pia kwa babu na bibi zangu kule.Kuna Christmas moja niliilia kwenye kota za police, sitosahau. Ilikuwa napenda sana kwenda kusherekea Christmas na mwaka mpya kwa bibi ifakara. Sasa kipindi hicho hakuna usafiri zaidi ya train ya tazara. Hakuna barabara za kueleweka dar-ifakara unaweza hata tumia wiki kwa gari. Tar 24 nikapandishwa train nakumbuka nilikuwa mdogo saana ila kuna mtu nilikabidhiwa anishushe ifakara pale nitapokelewa na bibi. Sijui nilijichanganya vipi nikapoteana naye kwenye train, na safari ilikuwa usiku. Chuma imetembeeaa, kumbe nimepitiliza kituo nikaja kuuliza kumbe tumeshapita kama vituo vitatu nyuma almost 80kms, usiku kama wa saa saba. Abilia wakamwambia TTE, anishushe sehemu inaitwa mngeta. Ni giza sijawahi ona mvua inanyesha. Nimeshikilia mikate ambayo nilimbebea bibi.
Kile kisehemu ni mji mdogo sana, train ilivyoondoka watu wote wakapotea nikabaki nimekaa karibu na ofisi ya mizigo nalia tu. Akaja askari mmoja sijui wa tazara yule, nikamuelezeaa. Akanichukua akanipeleka kwake nalia tu hata kula sili, nimekumbatia mikate yangu. Simu hakuna ikabidi kesho yake wakatumia zile simu za tazara kupiga ifakara wakaunganisha na simu za posta, ndo nikaongea na bibi hiyo ilikuwa next day jioni. Watoto wakawa wamenizunguka wananishangaa tu nimepotea.
Nilikataa kula chakula chao nilikula tu mkate kidogo, jioni wakanipeleka kanisani (catholic) lipo milimani hivi. Kule nilibahatika kuna gari ya mapadre lilikuwa linaenda ifakara kesho yake.
Nilifika kwa bibi nimechoka sana na mikate imeharibika. Ile Christmas ilikuwa ya mateso sana kwangu
Hata majina sikumbuki sahiv, ila alikuwa anaishi karibu na posta (zamani) pale round about (tulikuwa tunaita mwenge wa bandia) mbele kidogo. Sijui kama sahivi kuna mazingira hayo. Maana sasa yapata zaid ya miaka 25Bibi yako anakaa sehemu gani? Hapo ifoza mimi pia kwa babu na bibi zangu kule.
Nimecheka sana, kwani kazi yake inawahusu nini? Na kueleza lazima usimame?
Hahaha watu wanavituko sana, hii imenichekesha sana leo.
Mkuu japo inaumiza Sana ila nimecheka Sana dahSimulizi ya pili
Hii ni 1994. Nimefanya Kazi kwa mtu kule SABASABA mpaka tar.20.. Nikaambiwa mshahara tar 23.. Kumbe tajiri kajipanga kuondoka tar 22.. Nafika kwake tar 23 naambiwa kaondoka jana kwenda mkoani😭 sikuwa na pesa kabisa
Aliyenikoa ni bibi mmoja aliyekuwa anauza maji pale SABASABA (sikuwahi kumlipa wema wake ule) alinipa shiLingi 5000 ilikuwa kubwa sana kipindi Hicho
Sasa ni tarehe 23 natakiwa kusafiri tar 24 kwenda kijijini kwa ajili ya Xmas
Basi kujiongeza nikapata mchongo wa maembe huko Chanika Mvuti
Nikafanikiwa kupata 20 ya mkopo mahali.. Nikawa na 25 sasa.. Nikaenda zangu Mvuti
In short mpaka saa tatu usiku nilikuwa Buguruni na tenga langu la maembe nikiwa nimeshatumiq kama elfu 22 hivi gharama zote na matarajio ni kupata 45 hivi
Ugeni kwenye biashara jambo baya sana.. Nikaambiwa yale maembe yangu yanaweza kununuliwa kwa jumla elfu 25 tuu ama sivyo nikomae mwenyewe niuze mojamoja
Baada ya mabishano ya muda mrefu nikashindwa mimi inabidi nikubaliane nao
Sheshe likaja kwenye kuyamwaga chini yakaguliwe😭😭😭
1. Nilichomekewa maembe mabovu almost robo tenga
2. Waliweka majani mengi chini ya tenga..
Niliambulia Shilingi elfu 9000.tuu.
Ndo ujue humu tupo wazee wengi tuMbona hizo stori zenu za miaka wengine bado hatujazaliwa🤕
Ok napajua huko km unaelekea kivukoni. Sawa rudi sasa hivi aisee siyo ile ya miaka ya 90 huko imechangamka sana na kuendelea pia. Miye nimeamua kila mwaka narudi kukaa hata wiki moja alafu nasepa zangu.Hata majina sikumbuki sahiv, ila alikuwa anaishi karibu na posta (zamani) pale round about (tulikuwa tunaita mwenge wa bandia) mbele kidogo. Sijui kama sahivi kuna mazingira hayo. Maana sasa yapata zaid ya miaka 25