Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakaππππ
Hapo ndo unaweza kuanza kuwaza kwani Mungu yupo kwa ajili ya watu gani? So sadSimulizi ya pili
Hii ni 1994. Nimefanya Kazi kwa mtu kule SABASABA mpaka tar.20.. Nikaambiwa mshahara tar 23.. Kumbe tajiri kajipanga kuondoka tar 22.. Nafika kwake tar 23 naambiwa kaondoka jana kwenda mkoaniπ sikuwa na pesa kabisa
Aliyenikoa ni bibi mmoja aliyekuwa anauza maji pale SABASABA (sikuwahi kumlipa wema wake ule) alinipa shiLingi 5000 ilikuwa kubwa sana kipindi Hicho
Sasa ni tarehe 23 natakiwa kusafiri tar 24 kwenda kijijini kwa ajili ya Xmas
Basi kujiongeza nikapata mchongo wa maembe huko Chanika Mvuti
Nikafanikiwa kupata 20 ya mkopo mahali.. Nikawa na 25 sasa.. Nikaenda zangu Mvuti
In short mpaka saa tatu usiku nilikuwa Buguruni na tenga langu la maembe nikiwa nimeshatumiq kama elfu 22 hivi gharama zote na matarajio ni kupata 45 hivi
Ugeni kwenye biashara jambo baya sana.. Nikaambiwa yale maembe yangu yanaweza kununuliwa kwa jumla elfu 25 tuu ama sivyo nikomae mwenyewe niuze mojamoja
Baada ya mabishano ya muda mrefu nikashindwa mimi inabidi nikubaliane nao
Sheshe likaja kwenye kuyamwaga chini yakaguliweπππ
1. Nilichomekewa maembe mabovu almost robo tenga
2. Waliweka majani mengi chini ya tenga..
Niliambulia Shilingi elfu 9000.tuu.
Hahaha kuna mila na desturi zina dharililisha utu wa mtu.Sinyanyuki niuweniπ
Safi sana, huo ndio uwanaume.Sinyanyuki niuweniπ
HahahhaSafi sana, huo ndio uwanaume.
Kuwa na mali nyingi haumpi mtu ufalme au mamlaka kudharilisha mwenzake.
Kaweka mguu chini , sinyanyuki niuweni.
Ni changamoto.. Imagine kapambana pengine mwaka mzima na hata hiyo nauli ya kurudi home kakopa halafu anakutana na kitu motoπHahaha kuna mila na desturi zina dharililisha utu wa mtu.
Yeye afanyacho huko Dar ni mambo yake binafsi, kwanini wao wadhani anao wajibu kuwaeleza wao, na eti lazima asimame wakati akijieleza?
Duh! Mwalimu alikula hasara ya Karne akaona iswe taabu akaamua kuacha na KAZI ππππππ! Umenimbusha mwaka 2006 nikiwa nimejishikisha kibarua cha kufundisha shule moja Dar maarufu ya private ya wakatoliki. Basi, katika zungumza zungumza muda wa chai ikatokea hoja ya biashara ya kununua mbuzi mikoani na kuzileta Dar machinjioni Vingunguti na kuziuza kwa bei nzuri. Yaani mikoani mbuzi unamnunu elfu 5 hadi 8 lakini ukimfikisha Dar bei ni kuanzia 30 elfu hadi 60. Mwalimu mwenzetu kajaa mazima sijui hela alizitoa wapi kapakia lory. Kipindi hicho kilikuwa kipindi cha mvua daraja la Luvu likafurika magari hayapiti mbuzi kwa wiki mbuzi wengi wakadhoofu na kufa. Kwa ufupi hakuambualia hata senti na mwisho wa siku akawa haonekani kazini mpaka natoka pale sikuwahi kumuona!
Unajua hata kama mtu anataka kukusaidia usikubali akakudhalilisha. Kama nia yao ni kumsaidia, wampe huo msaada basi waanze upya, wamuulize matokeo mwakani.Hahahha
Ni changamoto.. Imagine kapambana pengine mwaka mzima na hata hiyo nauli ya kurudi home kakopa halafu anakutana na kitu motoπ
Hahaha ningekuwepo ninge mnunulia beer mshikaji, big up kwake.ππππUnajua hata kama mtu anataka kukusaidia usikubali akakudhalilisha. Kama nia yao ni kumsaidia, wampe huo msaada basi waanze upya, wamuulize matokeo mwakani.
Wao hawajajieleza wanafanya nini huko waliko, hakuna aliyewauliza. Mwamba kaenda nyumbani kama wao walivyokwenda, wafurahi, wasalimiane, hayo mengine waulizane private, na kila mtu aendelee kivyake.
Lakini haya mambo ya kupeana MIC halafu mtu anakwambia tuambie huko Dar es Salaam unafanya nini, sio poa kabisa.
Nimependa msimamo wake, Yani ni zile kwamba "maisha yangu ni yangu, nani kakwambia nataka kuwa kama wewe, hata kama una good life?"
Jamama mmoja nasema nyie mnao fanikiwa punguzeni ushauri, siyo kila mtu ana waona nyie ni wamaana, hivyo msidhani kila mtu anapenda kuwa kama nyie, au kufanya mfanyacho.
Ana maliza kwa kusema "To hell with your good life" Ukivaa suti ni mapenzi yako, mimi napenda jeans. Ukila kuku ni mapenzi yako mimi napenda matembele, your life your choice.
Hahaha ningekuwepo ninge mnunulia beer mshikaji, big up kwake.
Umepitia mengi sana kwenye maisha, na kwa story zako inaonekana ni mkubwa wangu, mwaka ambao upo chuo mimi bado nilikuwa dereva wa sinia kwa wazaziLife has so much to tell
π€£π€£π€£ wewe utakuwa mtoto sana. Sisi nyumbani kwetu tunapikia gas tangu miaka ya 1980s!!!Mwaka 2000 mlikuwa mnapikia gas? ππ