Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Nimewahi kuwa muumini wa dini fulani kubwa ulimwenguni. Nilisoma kidogo basic ya dini ile.
Ile dini lengo lao ni moja tu, nalo ni kupata pepo ya Mwenyezi Mungu. Baadaye nikapata Neema ya kuwa Mkristo.
Ukristo yaani kuwa mfuasi wa Yesu ni jambo kubwa, la neema isiyo na kifani.
Ila nasikitika kusema kuwa watu wengi makanisani si wa Kristo. Yesu hawatambui kwa mizani yake. Hawajui kabisa, anawafahamu tu kuwa wapo makanisani wanaimba, wanatoa sadaka, wanafanya hili na lile lakini Yesu hawajui.
Wengine ni wachungaji, maaskofu n.k lakini Yesu hawajui.
Naongea katika Roho, watu watubu wamgeukie Mwokozi , yeye ni mwepesi wa kusamehe, si mwingi wa hasira.
Kwanini nasema watu wengi wanaitwa Wakristo lakini Yesu Kristo mwenyewe hawajui?
Kwasababu misingi yao tangu siku ya kwanza wanahubiriwa na kuamua kumkiri Yesu ilijengwa juu ya Mali, afya, promotion na vitu vingine ambavyo hata kabla ya kuja Yesu mwanadamu alikuwa na urahisi tu wa kuvipata vitu hivyo kwa kufuata sheria ya Musa. Suala la ufalme wa Mbinguni limekuwa si kipaumbele tena.
Yesu anamtambua tu yule muumini ambaye ukiupasua moyo wake jibu utakalolikuta ndani ni moja tu "NIMEMFUATA YESU ILI NIENDE MBINGUNI".
Kama kuna kuponywa sawa , kama sitaponywa sawa.
Kama kuna kubarikiwa vitu vya duniani sawa, kama hamna baraka sawa.
Kama kuna KUOLEWA sawa, kama sitaolewa sawa.
Kama nitapata kazi sawa, kama sitapata kazi .
Lakini sasa ukisikiliza maombi ya watu wa kanisani wengi yamebezi kutaka kuinuliwa, kupata kazi, kupata afya, kupata pesa n.k
Wamesahau kabisa kuwa Yesu hajawekwa msalabani kwasababu ya material things.
Lengo la Yesu kufa msalabani ni moja tu nalo ni kuwavuta watu wote walio willing wafike mbinguni jambo ambalo kabla ya kifo cha Yesu lilikuwa gumu.