KSh8,000 Kupiga Shoot Nairobi? Sheria Mpya Yazua Gumzo

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
469
Reaction score
95
Sheria hiyo mpya imeweka ada ya KSh8,000 kwa kila commercial filming session ya local production, huku production teams kutoka nje zikitozwa KSh50,000. Music video production itagharimu KSh10,000, huku content creation studios zikitozwa KSh40,000 kwa mwaka.

Influencers wanaoandaa monetised au ticketed events watatakiwa kulipa KSh10,000 kwa kila event. Local streaming platforms zitatozwa KSh100,000 kwa mwaka, digital content platforms KSh80,000, television stations KSh200,000 na radio stations KSh150,000.

Hatua hiyo imezua mjadala miongoni mwa creatives, hasa ikizingatiwa kuwa mwaka 2022 utawala wa Gavana Johnson Sakaja uliwaondolea freelance photographers na filmmakers ada za Single Business Permit, hatua iliyowasilishwa wakati huo kama njia ya kupunguza vikwazo kwa sekta ya ubunifu.

Hata hivyo, baada ya wasiwasi kuibuka, Sakaja amefafanua kuwa ordinary social-media creators na influencers wanaotengeneza content zao za kawaida si walengwa wa ada hizo.

Amesema county inalenga zaidi professional commercial productions zinazokuja na crews kubwa, vifaa, magari na wakati mwingine kuhitaji matumizi maalum au kufungwa kwa public spaces.

Kwa hiyo, swali kubwa sasa si tu “content creator atalipa?” bali county itawezaje kutenganisha ordinary creator na commercial production bila kuacha nafasi ya harassment au confusion wakati wa enforcement?
 

Attachments

  • eastleighvoice-co-ke-2026-august-18-081829.webp
    23.1 KB · Views: 33
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…