Ku Klux Klan

Ku Klux Klan

Darnes 2016

Member
Joined
Aug 5, 2018
Posts
19
Reaction score
7
View attachment 983413View attachment 983414

FIRST KLAN 1865-1871

Kama nilivyoahidi nitachambua kiundani kuhusu hili kundi lenye historia mbaya sana ktk ainabinadamu. Leo nitaanza na hii First Klan

Abraham Lincoln, rais wa 16 wa Marekani baada tu ya kuapishwa Machi 4th 1861 kuwa rais mpya wa Marekani aliadhimia kuwapa uhuru watumwa wote. Hilo lilikuwa jambo hatari na baya ukitegemea hasa yale majimbo ya kusini yalikuwa yamejibase sana kwenye kilimo sasa kuwaweka huru watumwa inamaanisha mashamba yao hayangekuwa na wafanyakazi hali ambayo ingechangia uchumi wao uporomoke. Hivyo hakukuwa suluhu nyingine isipokuwa kupinga huo msimamo wa Lincoln na hapo ikazaliwa hiyo ambayo ilikuja kuitwa baadaye American Civil War.

Majeshi ya Lincoln yakiongozwa na General Ulysses S. Grant(ambaye alikuja kuwa baadae rais wa 18 wa Marekani) yalishhinda vikali vikosi vya majimbo ya kusini na kupelekea watumwa wote kuwekwa huru, kupewa haki za msingi za kibinadamu na kuwa kama raia wa kawaida.

KUUNDWA KWA FIRST KLAN

Baada ya rais Abraham Lincoln kupigwa risasi mnamo April 4th 1865 na kijana aliyekuja kufahamika kama John Wilkes Booth, nchi ilichafuka upya tena baada ya makamu wake Andrew Johnson kutokuonyesha uwezo wa kusimamia serikali yake ipasavyo.
Ifahamike kuwa Abraham Lincoln ndie aliyekuwa rais wa kwanza toka chama cha Republican Party kutawala.

Baada ya kifo cha Lincoln, Andrew Johnson ambaye alikuwa ni mdemocrat wa asili ya North Carolina moja ya yale majimbo ya kusini serikali yake haikutoa ulinzi wa kutosha kwa watumwa wa zamani. Hali iliyochangia kutokea kwa kundi hili la KKK (Ku Klux Klan)

Kundi hili liliundwa kati ya December 1865 na August 1866 mjini Pulaski, jimbo la Tennessee. Kundi hili liliundwa na maofisa sita wastaafu wa liliokuwa jeshi la kusini. Neno Kuklux linatokana na neno Kyklos linalotafsiriwa Circle(duara).

Muda mfupi tu baada ya kuanzishwa kundi hili lilianza propaganda za kuendekeza ukuu wa ngozi nyeupe (white supremacy), ukatili wa hadharani dhidi ya watu weusi, kuunguza nyumba, mashule, na makanisa ya watu weusi, Waliwaua na kuacha miili yao barabarani, kuwanyonga na kuwaacha wananing’inia kwenye miti kandokando ya barabara.

Isitoshe waliwatendea unyama huohuo wazungu wenzao wanachama wa Republican Party iliyokuwa na muelekeo wa kuwapa uhuru wa kupiga kura watu weusi.

Mwaka 1867, KKK walifanya kikao cha kitaifa mjini Nashville, Tennessee ili kujadili muelekeo wao mpya na kumpata kiongozi atakayewasimamia kitaifa. Hapo ndipo alipochaguliwa Gen. Nathan Bedford Forrest kuwa kiongozi wao mkuu wa kwanza au First Grand Wizard kama wanavyomuita wenyewe.
Huyu bwana Bedford ndiye aliyeleta wazo la Castrations (au kuwakata kende, pumbu) wanaume weusi ili wasizidi kuzaana.
Kwa kuwa bwana Forrest alikuwa na cheo serikalini aliipinga vikali ile sheria ya KEEP AND BEAR ARMS dhidi ya watu weusi. Sheria hii inamruhusu mtu kumiliki silaha kama njia ya kujilinda. Alijtoa hoja ya kwamba kwa kuwa mtu mwenye ngozi nyeusi akipewa haki hii basi atafanya mambo mabaya zaidi kama ilivyo rangi mbaya ya ngozi yake. Vile vile alihusisha mtu mweusi kama mtu duni(fake) aliyeletwa duniani kumtumikia mtu mweupe(mzungu) Hoja yake ilipingwa na hivyo kila mtu akapewa haki ya kumiliki silaha kama njia ya kujilinda. Inaripotiwa katika mji wa Bennettville, jimbo la South Carolina watu weusi wenye silaha waliunda kikundi chao ili kujilinda wao na maeneo yao.

MWISHO WA FIRST KLAN

Baada ya miaka miwili tu ya shughuli zao za kinyama wanamemba wa kundi hili walianza kuvaa makanzu marefu na mask usoni ili kujificha wasifahamike. Kwa kuwa mlengo wao wa kisiasa ilikuwa Democratic Party na rais Andrew Johnson aleyekuwa madarakani kipindi hicho alitoka katika chama hicho kwahiyo kufanya ule ukatili hadharani ingemaanisha wanaungwa mkono toka serikalini.

Katika jimbo la Alabama ilianzishwa harakati ya Anti-Kukluxklan. February 1871, Congressman Benjamin Franklin Butler kutoka Massachusetts aliunda sheria ilnayoitwa Civil Right Act of 1871(ambayo inatambulika tena Kama Ku Klux Klan Act). Sheria hii inapinga harakati zozote za kikatili dhidi ya watu wa jamii tofauti na yako. Sheria hii iliwazuia Ku Klux Klan kukusanyika au kufanya mikutano yao hadharani. Ililadhimisha kusitishwa kwa harakati zozote za kibaguzi dhidi ya watu weusi.
Baada ya sheria hii kutoka Wanakukluxklan au Klansmen kama wanavyoitwa walikataa kusambaratika au kusurrender au kuacha kufanya ukatili wao hali iliyomlazimu Ulysses Grant ambaye sasa alikuwa rais kuingilia kati na kutumia nguvu za ziada kuwasambaratisha. Alitumia majeshi yake kumkamata yeyote yule waliyemuhisi ni Klansmen na kumtupa lupango. Ukigundulika wewe ni klansman unapigwa faini ya dola kati $2900 na kifungo cha kati ya miezi mitatu hadi miaka mitano. Msako huo ulitosha kuwasambaratisha kabisa.

Mwishoni mwa December 1871 Grand Wizard Nathan Bedford Forrest alitoa wito wa kuharibu na kusambaza kundi hili na kufikia February 1872 Ku Klux Klan hawakusikika kabisa.

NOTE: Baada ya kundi hili kusambaratishwa yalitokea makundi mengine kama White League, Red Shirts, Riffle Clubs, Sabber Clubs... ambayo yalikuwa na mlengo uleule waliokuwa nao KKK lakini hawa hawakuwa na nguvu sana kama KKK.



Wakati Vita Ya Kwanza Ya Ulimwengu inarindima Europe, kwenye sherehe ya Thanksgiving ya 1915, Georgia Marekani, bwana William Joseph Simmons anafanya mkutano mkubwa wenye lengo la kuifufua KKK [emoji849]

Je ni hatma gani kwa watu weusi? Nifuatilie...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
God bless you kwa historia nzuri na inayoonyesha kuwa kutakuwepo ushindi kwa wenye haki.......
 
Back
Top Bottom