Ndo yuko hivo, basi. Inabidi watu anaokaa nao au kufanyakazi nao wamfahamu. Si kwamba kila anayetabasamu anakuwa kafurahi, au anayelia anakuwa kapatwa na msiba au uchungu. yaweza kuwa kinyume chake. Watu wa namna hii yafaa kuwafahamu kwa kuingia ndani zaidi ya kile kinachoonekana kwa macho: kujua tabia yake gestures zake. Nakumbuka nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari, mwalimu wangu mmoja alipokuwa na furaha alikuwa serious kweli. Alipokuwa akikasirika alikuwa anatabasamu (kama huyo dada) - anaonesha uso wa 'furaha'. Tukamjua kwamba akitabasamu ujue hali ni mbaya: kaa chonjo!