Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Huwa na tatizo la kupenda na kutamani wanawake wazuri wazuri; nimejaribu kulikemea hili pepo, lakini haliondoki.
Mwezi uliopita, nikiwa kwenye mishe mishe zangu, nikakutana na dada mmoja, ni mtu mzima, na kwa uzuri aliokuwa nao, ukanishawishi nipambane niweke kituo; tukasalimiana, nikawa najaribu anielekeze maeneo fulani; ila lengo langu ni kupata namba.
Baada ya kunielekeza; nikamshawishi, na akanipatia namba.
Tukawa tunawasiliana, na kuendelea kufahamiana zaidi. Hajaolewa ila ana mtoto mmoja, pia ameajiriwa kwenye kampuni ya mtu binafsi.
Nikatafuta jumamosi moja, nikamtoa 'out' ili tuweze kuzungumza zaidi. Mbaya zaidi, wote ni wanywaji, tukawa tunapiga chupa na vitafunwa huku tukibadilishana mawazo.
Katika mazungumzo, nikaona ameanza kubadilisha sauti, na kuleta sauti ya kudeka deka, mara akaanza kuniita 'baby'; kusikia hivyo, nikajisemea kimoyo kimoyo, hili ni zigo langu.
Akasema,''baby, natamani niache kazi; kwa kasababu hii kazi ninayoifanya, inanichosha sana, na sifurahii maisha, nakuwa mtumwa''. Nikamuuliza unata ufanye nini, ukiacha kazi? Akanijibu biashara.
Akaendelea,'' Baby, naomba uniongezee mtaji''. Nikamuuliza kiasi gani? Akaniambie milioni 7.
Mwili ukashtuka ghafla, nikaanza kutafakari, mi nitanufaika na nini kama nitatoa hiyo fedha.
Nikamjibu; nizalie kwanza mtoto; ukibeba mimba ikiwa na miezi minne nakupatia tatu, na ukijifungua namalizia nne.
Akaniambia, haina shida.
Kwa nini nilimuambia hivyo? Kwa sababu hawa watu wakifanikiwa huko mbele huwa wanasahau walikotoka; ni bora uache alama.