Mkuu kujitosa katika kitu chochote bila preparation sio ujasiri bali ni upunguani..., katika kila maisha yako inabidi kuwa na plan B, na kufanya calculated risks.., na hapa tunaongelea miradi na kujiongezea kipato ila wewe unachanganya na running multi million corporations.., hivi kuna ubaya gani kama huyu mtu anavuta mkwanja wa kutosha kazini kwanini asianze kwanza part time (gaining experience) na kufanya investments kwenye vitu kama real estate n.k. vitu ambavyo anaweza kutumia leverage (efforts of others) to make money, pia kufanya investments tofauti (not putting ones eggs in one basket) hence anakuwa ame-hedge risk, baada ya hapo hata atakapoacha kibarua chake will have somewhere to fall upon...,
Akifukuzwa kazi amefukuzwa kazi hio ni part ya maisha sio sababu anaweza kufukuzwa kazi ndio aache kazi leo kabla ya kujitayarisha.., cha maana narudia (kama kazi yako ina kipato cha kutosha) tumia hicho kipato ku-hedge risk kwa investments ndogo ndogo hata utakapoacha kazi kunakuwa na fedha ya kujihifadhi in a rainy day..., sio unaamua kuacha kazi leo wakati hata pesa ya mwenye nyumba hujamalizia kumlipa.
Huu msemo wa kuchoma meli ni just msemo.., huyo jamaa yako alichoma kabisa na vyeti vyake au ?..., sababu anaweza akakwambia hivyo ila deep down when push comes to shove angeweza kuanza kutuma applications tena (if he is employable), pia cha maana ni kwamba aliacha nini na kwenda kufanya nini ? (hapo keyword ni kufanya nini.., sio kuamua kuacha kazi kama CEO fulani alafu kuamua kwenda kuendesha bodaboda yake.., sababu hata hii ni biashara)