CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Ndugu Chasha suala la kuongeza elimu while doing business ni jambo la kawaida,wengi imewezekana na jamaa kasema wife yupo nyumban so ni msaada tosha...kuongeza elimu kuna faida nying,kama ni muajiriwa utazijua,baadhi tu ni kipato kuongezeka,heshima,kukuza uelewa na assurance ya kuongeza mafao pale utakapostaafu.
Mkuu kujitosa katika kitu chochote bila preparation sio ujasiri bali ni upunguani..., katika kila maisha yako inabidi kuwa na plan B, na kufanya calculated risks.., na hapa tunaongelea miradi na kujiongezea kipato ila wewe unachanganya na running multi million corporations.., hivi kuna ubaya gani kama huyu mtu anavuta mkwanja wa kutosha kazini kwanini asianze kwanza part time (gaining experience) na kufanya investments kwenye vitu kama real estate n.k. vitu ambavyo anaweza kutumia leverage (efforts of others) to make money, pia kufanya investments tofauti (not putting ones eggs in one basket) hence anakuwa ame-hedge risk, baada ya hapo hata atakapoacha kibarua chake will have somewhere to fall upon...,
Akifukuzwa kazi amefukuzwa kazi hio ni part ya maisha sio sababu anaweza kufukuzwa kazi ndio aache kazi leo kabla ya kujitayarisha.., cha maana narudia (kama kazi yako ina kipato cha kutosha) tumia hicho kipato ku-hedge risk kwa investments ndogo ndogo hata utakapoacha kazi kunakuwa na fedha ya kujihifadhi in a rainy day..., sio unaamua kuacha kazi leo wakati hata pesa ya mwenye nyumba hujamalizia kumlipa.
Huu msemo wa kuchoma meli ni just msemo.., huyo jamaa yako alichoma kabisa na vyeti vyake au ?..., sababu anaweza akakwambia hivyo ila deep down when push comes to shove angeweza kuanza kutuma applications tena (if he is employable), pia cha maana ni kwamba aliacha nini na kwenda kufanya nini ? (hapo keyword ni kufanya nini.., sio kuamua kuacha kazi kama CEO fulani alafu kuamua kwenda kuendesha bodaboda yake.., sababu hata hii ni biashara)
Mkuu swala la kuacha kazi si kwamba ni mpaka uwe na uhakika wa 100% wewe hutakaa uelewe na najua wewe ni moja wa wahanga wa kazi, ni vigumu sana na mwajiriwa kutoa ushauri wa mtu kuacha kazi, ni kitu ambacho hakipo.
Again point yangu ipo pale pale aliacha huo ualimu ili aende kufanya nini (biashara ipi), sababu hata mimi ninamjua mwalimu mmoja aliacha kazi akaamua kuanza kuuza electronics, matokeo yake sababu ya biashara ya huku ilivyo watu wasumbufu, wanataka bei ndogo na uduni wa products za China hivi sasa anagongea hata nauli..., wakati kipindi kile alikuwa anafanya biashara ya kufundisha hata tuition na hata angeweza labda kutunga na kuuza materials ya masomo yake ingekuwa a better alternative, pia kumbuka huyo Muguku kuacha kwake Ualimu angeweza anytime akaenda sehemu na kupata kazi sio kwamba alichana vyeti vyake.Jaribu kusoma story ya MUGUKU, huyu jamaa sasa marehemu aliacha kazi ya ualimu na kila mtu alimshangaa nan kufikia mhali Wazazi wake kuamini kabisa mtoto wao kachanganyikiwa but yeye alikuwa amekwisha amua moja.
Yees hao watu wanaoacha kazi za mamilioni wanakuwa tayari wameshaweka a plan in hand wanakuwa na plan B tayari sababu baada ya kusave hayo mamilioni hata kwa miaka mitano wanakuwa tayari wamesave vya kutosha na kuweka investments nyingine ndogo ndogo za kuweka mambo sawa.Ukikalia kwamba mimi ni bosi, natumia gari la shirika na kazalika huta kaa uwe na hii spirit, Watu wanaacha kazi za mamilioni na kwenda kuanza kazi za kuingiza elfu kadhaa badala ya mamilioni, usikalie kwamba uache kazi leo halafu wiki ijayo uwe tajiri make ndo za wabongo, anataka aanze leo then kesho awe biulionare, MUGUKU pamoja kwamba watu walimshangaa ila baadae mpaka anafaliki alikuwa kwenye top 5 ya matajiri wakubwa kabisa nchini Kenya,
Ofcourse ni process na safari ndefu that's why plan ni ya lazima, alafu hao wa kina Edson alikuwa ni inventor ambaye alikuwa na team ya watu wabunifu (at one time even Tesla alimfanyia kazi) kwahio kuanza kumfananisha willy nilly na mtu aache tu kazi for the sake ya kuacha kazi nadhani ni silly.., Pia inabidi tuangalie kwanini mtu anafanya kitu in the first place.., mwingine mapenzi ya kitu (feel good factor) mfano kufundisha..., mwingine mfano anachokifanya kinahitaji institution fulani ili akifanye..., au utasema pia mtu kama Messi aache kucheza mpira aende akafanye biashara yake (ni biashara ipi ambayo ataingiza pesa kama ile yeye kama Messi) au utamshauri aendelee kucheza huku anatumia kujulikana kwake yeye kama product ili aendelee kuingiza pesa through sponsorship na matangazoUjasirinali ni process ni safari ndefu sana na uoga ndo adui mkuwa sana, mbona wakina Edson walifeli mara nyingi but walikuja kufanikiwa, usikae kuwaza mishahra mikubwa kwamba ndo ikufanye usiache kazi,
Kwahio labda unamshauri mtu aache kazi ili kwanza aanze kuuza karanga ili baadae akue na kusambaza africa nzima ?, Au hii kazi anaweza kufanya research ya masoko na kutafuta mauzo na kuweza ku-supply kwa watu in container loads na polepole kujenga mahusiano na watu..., nadhani mkuu inabidi ujiulize tofauti ya kufanya kazi effective na kufanya efficiently...Hivi kwako biashara ni ipi? Hizi kampuni zote unazo ona leo zilianza chini kabisa, hakuna kampuni hata moja hapa Duniani iliyo ibuka ghafla, makumpuni yametoka mbali sana, Tatizo wewe unazani biashara ya Toyo sio biashara, hakuna biashara kubwa wala ndogo, mtu anaweza anza hata kuuza karanga na baadae akaja kuwa msambazaji wa karanga hata Africa nzima, ishu ni wewe uko commited kiasi gani,
Mkuu nasema tena inategemea unaacha nini na kwenda kufanya nini wewe kama CEO unaweza kuacha kazi yako na kufungua firm yako na kufanya kile kile kwa makampuni tofauti kwa ku-outsource kazi yako ila sio uache kazi ya kipato kikubwa na kwenda kufungua genge la kuuza nyanya (hio sio efficiency)..., ila kama wewe ni mama lishe umeajiriwa unapika na kuuza chakula kwa wateja (mtaji sio mkubwa) ni bora na rahisi kuanza kupika na kuwasambazia wateja walewale chakula kilekile ila tofauti hapa profit itakuwa kubwa.Wewe ma CEO kwako ndo unaona watu wasio takiwa kuacha kazi ila wafagiaji ndo wanatakiwa kuacha, Mkuu naomba mimi niishie hapa make hutakaa unilewe milele
In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. – Bill Cosby
Kwahio labda unamshauri mtu aache kazi ili kwanza aanze kuuza karanga ili baadae akue na kusambaza africa nzima ?, Au hii kazi anaweza kufanya research ya masoko na kutafuta mauzo na kuweza ku-supply kwa watu in container loads na polepole kujenga mahusiano na watu..., nadhani mkuu inabidi ujiulize tofauti ya kufanya kazi effective na kufanya efficiently...
Mkuu nasema tena inategemea unaacha nini na kwenda kufanya nini wewe kama CEO unaweza kuacha kazi yako na kufungua firm yako na kufanya kile kile kwa makampuni tofauti kwa ku-outsource kazi yako ila sio uache kazi ya kipato kikubwa na kwenda kufungua genge la kuuza nyanya (hio sio efficiency)..., ila kama wewe ni mama lishe umeajiriwa unapika na kuuza chakula kwa wateja (mtaji sio mkubwa) ni bora na rahisi kuanza kupika na kuwasambazia wateja walewale chakula kilekile ila tofauti hapa profit itakuwa kubwa.
Hapana usiishie hapa..., hapa tueleweshane kwa hoja.., naomba ujifanye wewe ndio huyu Bwana mwenye laki tano yake kwa mwezi unamwambia aache kazi leo akafanye biashara gani hio inayohitaji muda wake 100%, ambayo asingeweza kuanza polepole na kwa kujitayarisha kwa investments ndogo ndogo part time
Kwani Nyanya sio Biashara? Usikalili kwamba biashara ya heshima ni lazima uwe unauza Magaru Used kutoka Japani, Uuze sijui simu, inategemeana Idea yake imekee vipi, anaweza hata akaanza project ya kuuza karanga, ila all in all inategemeana yeye anamalengo gani,
Wewe unazania akianza kuuza nynya ataonekana mjinga?
Aongeze elimi ili iweje? apate mshahara mkubwa au, Ujasirimali si ishu ya kitoto huwezi practise vitu viwili at the same time ni lazima uamue moja,
Wakuu, endeleeni kubishana wengine tunanufaika sana na mbishano huu.. Pande zote mbili Zinaongea point zenye kujenga... Tafadhari Rudini tena tuendelee na shamba darasa.
Unaonekana ni muoga saanaMkuu nisha sema kuacha kazi na kuingia kwenye ujasirimali si ishu ya kitoto, najua watu wanahofia kuchekwa, kutengwa, kuachwa na kazalika, hivyo kama hizo ndo sababu ni bora mtu akakomaa na kazi tu, Kwenye biashara kuna risk hata ukisema biashara ikue kwanza ipo siku unaweza jikuta biashara yako imesambaratika unatakiwa kuanza mwanzo, je hapo familia haitasambaratika? hizo ni sababu mfu.
Kinacho takiwa ni kukaa na kuelimisha familia yako, kwa sababu kama ishu ni familia kusambaratika je ukifukuzwa kazi itakuwaje?
Kuchoma Meli moto ni kazi moja ngumu sana yenye uchungu wa hali ya juu, nakumbuka kuna jamaa angu alifanya zoezi kama hili la kuacha kazi na kuingia kwenye business huku akilia sana, ila alisha amua moja, hivyo ni lazima uamue moja,