Kuacha kuongeza mshahara ni kosa kubwa

Ukisomesha watu namba ni lzm nawe uisome hii ni kanuni, usitafute mchawi
 
Yani hajaonza
Acha kubwata wewe . Hujui lolote kuhusu utumishi wa umma, unaleta ujinga wako wa UK. Ili uonekane unajua kumbe mjinga tu.
Kupandishwa/ kuongezwa mshahara kunakwenda sambamba na kupandishwa watu madaraja na vyeo ambayo vina muathir mtumishi wakati wa mustafi hujui hilo???
Huko uk kuna nyumba za serikali hapa zipo? Mtumishi aliyepanga nyumba kodi unapanda kila mwaka na mshahara haupandi unaongea uzuzu wako hapa
 
Wafanyakazi wameongezewa mishahara chungu nzima

Mwambieni na Mbowe akuongezeeni hapo ufipa
 
Watumishi wa serikali wako wangapi!?

Wanalipwa sh. Ngapi kwa mwaka!?

Wanachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa!?

Wanategemewa na watu wangapi!?

Lengo sio kubishana.. wala kuona wivu wa waajiriwa.. unajuaje ..je kama mimi nimeajiri!? Inaonekana unahasira.. lakini ujenzi wa chochote unahitaji kujitoa.. sasa hatuwezi kujenga nchi wanaojitoa ni wakulima tu na wafanyabishara... Sote tujitoe tukikaa kula kusiwe na ksimangana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Da Da we jamaa una akili Sana.
Wengi hawajui ukweli huu.
Ukiondoa huo mzunguko wa fedha uliosema Kuna huduma Bora itokanayo na kuwa na maslahi Bora.
Mfano waalimu,madaktari,manesi,Mapolisi wanaolipwa vizuri hutoa huduma nzuri,Bora na upendo juu.
Waalimu wanaolipwa vizuri Watoto wetu hupata elimu Bora.
 
Anachokisema ni uongo.

Miji yenye mzunguko mkubwa wa fedha ni miji ya wafanyabishara na wachuuzi.. ukija na nadharia hiyo unieleze how watumishi ambao hardly wanafika mil 2 na mishahara yao ni around trilioni moja kwenye uchumi mkubwa kama Tanzania wanakuwa major spenders!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wewe hujui kutofautisha Kati ya microeconomy na macroeconomy. Katika uchumi mdogo waajiriwa ndio game changers. Waajiriwa ndio kundi Tanzania ambalo hata mabenki linawaani, yaani wanakopesheka. Idadi ya kukopa benk na ukubwa wa pensions unategemea na ukubwa wa mshahara mtumishi analipwa kwa mwezi. Kama mtumishi hajaongezewa mshahara kwa miaka uwezo wake wa kukopa hela nyingi umepungua na hela inayokwenda kwenye mifuko ya hifadhi za jamii inapungua pia, hivyo kupunguza purchasing power ya mfanyakazi. Kama uwezo wa manunuzi ukipungua maana yake hata biashara zitadorora. Hapa ndipo watu watakapojidanganya kuwa wameounguza mfumko wa Bei, lakini sio kweli kuwa wameounguza mfumko wa bei bali watu hawana hela ya kumeet demands zao. Utakuta nyanya na matikiti yanaozea kwenye meza sokoni na shambani kwa mkulima sio kwasababu uzalishaji umeongezeka Bali watu hawawezi kumudu kununua nyanya japo wanazihitaji.

Hata kwenye bar wateja Ni wengi mwisho wa mwezi, hata madukani wateja Ni wengi mwisho wa mwezi , hata karo za shule malipo Ni makubwa mwisho wa mwezi , hata michango ya harusi ahadi zinalipwa nyingi mwisho wa mwezi, hata supermarket wanunuzi Ni wengi mwisho wa mwezi. Kwanini?

Ukweli Ni kwamba mheshimiwa alikosa ushauri mzuri kwenye hili, maana hata uwezo wa Askari kunywa pombe umepungua sana pia. Hivyo hata Askari lazima Kuna wanaosema hapana hiki, hata wale usalama wa taifa ambao walikuwa wakisafiri nje ya nchi wakati Mkuu wa nchi akisafiri nje nao pia uwezo wao wa manunuzi umeshuka maana hakukua na safari nyingi za nje Kama zamani.
 
Nyie ndio mnagawana keki ya taifa sio?
 
Shule hulipi ada,hiyo hela badala ya kulipa ada ongeza kwenye mshahara wako,bwawa la Umeme likiisha Umeme ukishuka bei,ile hela unayo save kutokana na umeme kupungua ongeza kwenye mshahara wako,
 
Swali langu ni kuwa hii trilioni moja ya watu milioni mbili pekee ndio inaendesha uchumi!?

Ndiyo inanunua matikiti yasioze, nyanya na kunde sokoni!?

Ni hawa watu milioni mbili tu watumishi wa serikali ndio wanaostabilize uchumi mdogo wa Tanzania!?

Ni hao tu watu milioni mbili wanaokula mazao ya kilimo!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ndio Hawa afande. Maana kundi hili lina wanajeshi, polisi, uhamiaji, usalama wa taifa, wauguzi, madakatari, wakusanya ushuru, walimu, wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, wazoa taka, marubani, nk ambao ndiyo injini ya uchumi. Kundi hili linaonekana dogo kwa maoni yako lakini ndio uti wa mgongo wa taifa na uchumi kwa ujumla, Kama kundi hili ukilichanganya ubongo hata hayo makundi mengine hayatafua dafu.
 
Unajua Mishahara ya watumishi ni kiasi gani kwa mwaka!?

Tozo zao za kodi Unazifahamu!?

Unaweza kusema bila kupepesa Tozo zinazotoka kwa wafanyakazi wa serikali ni kubwa na nyingi kuliko kundi jingine lolote!?

Na unaweza kusema bila shaka pato la wafanyakazi ndilo pekee linalotengeneza highest spenders nchini!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Unachotaka tuamini Ni kuwa watumishi Ni kundi ambalo sio muhimu sanakuliko mengine.
 
Unachotaka tuamini Ni kuwa watumishi Ni kundi ambalo sio muhimu sanakuliko mengine.
Nachotaka kuamini watumishi ni kundi muhimu kama makundi mengine. Na special treatment kama za kuongezwa mishahara zinaweza kuwa extended kwa makundi mengine pia.. kwa namna tofauti.. and once that happens watumishi wafurahie pia kwa niaba ya watanzania wa makundi mengine waliokumbukwa.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Shule hulipi ada,hiyo hela badala ya kulipa ada ongeza kwenye mshahara wako,bwawa la Umeme likiisha Umeme ukishuka bei,ile hela unayo save kutokana na umeme kupungua ongeza kwenye mshahara wako,
Na FAO LA KUJITOA?

#YNWA
 
Nikukumbushe tu kuwa mtumishi ni yule mtu ambae anapangiwa na mwajiri wake anze na kumaliza kazi muda, siku, mwezi na mwaka gani. Kwa mtumishi wa serikali yeye anapangiwa hivyo na serikali kwa manufaa ya makundi mengine. Hapa unaongelea watu kama walimu, madakatari, wakusanya kodi, polisi, wanajeshi, zima moto, wahasibu, makuli, nk. Hawa mara nyingi huwa wanapunzika na kufanya mambo yao binafsi siku 28 tu kwa mwaka. Kama mtu huyu utamruhusu afanye kazi nyingine kama vile kufuga kuku, samaki, bata au kuwa na kiosk, shamba au kitu kingine cha kumuongezea kipato basi utakaribisha huduma duni kwa anaowahudimia kwenye ajira yake mama. Kwa maana nyingine huyu mtumishi lazima amtegemee mwajiri wake kwa 99.9% kwa kipato chake vinginevyo malalamiko kwa wapokea huduma zake yatajitokeza tu.

Sasa mtu wa aina hii kutokumuongeza mshahara maana yake unamwambia asimtegemee mwajiri wake kwa 99.9% kiuchumi, akafanye shughuli za ziada kama kuendesha boodaboda, kufungua duka, kuuza karanga na ubuyu darasani, kutoza rushwa, ukahaba, kulima bustani na mashamba, nk ili kuziba pengo la mwajiri. Malalamiko ya wananchi kwa watumishi na huduma yataanzia hapo. Hii ni tofauti na makundi mengine ambayo yanafanyakazi zao kwa kujipangia wenyewe muda wa muamka na kulala, muda wakufanya kazi na kupunzika na nini cha kufanya na wapi kwa kwenda, kishinda na kulala kwa siku, mwezi na mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…