POTOSHI Kuacha kutumia sukari katika mlo ni tiba ya saratani?

POTOSHI Kuacha kutumia sukari katika mlo ni tiba ya saratani?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na video ya huyu jamaa naeleza kuwa mtu akitaka Saratani (Cancer) hana haja ya kutumia dawa zza hospitalini ili kutibu ugonjwa huo na badala yake anapaswa kuacha kula vitu vyenye sukari na Cancer hiyo itaondoka yenyewe.

Pia anaelezea kuwa mtu huyo anapaswa kupata kiwango kikubwa cha Oksijeni. Madai haya yana uhalisia kiasi gani?


1763100917643.png
 
Tunachokijua
Sukari ni aina ya wanga inayokuja katika miundo tofauti. Sukari imegawanyika katika aina mbili ya kwanza ni sukari iliyoongezwa ambayo hupatikana kwenye vinywaji vyenye sukari, vitafunwa vitamu, pipi, na vyakula vingine vilivyosindikwa. Na aina ya pili ni Sukari za asili ambazo hupatikana kwenye matunda, mboga zenye wanga, na nafaka.

Taasisi ya Cancer research Uk, inabainisha kuwa seli za saratani hukua haraka na kuongezeka kwa kiwango kikubwa na ili kufanikisha hilo zinahitaji nishati nyingi, hivyo zinahitaji 'glucose' nyingi na hapo ndiyo nadharia ya kwamba sukari inaongeza saratani ilipoibuka.

Lakini uhalisia haupo hivyo kwamba ukiacha kula sukari utaizuia saratani isiendelee kukua. Wanaeleza pia hakuna ushahidi wa kuthibitisha jambo hilo na hata hivyo seli hizo hazihitaji tu 'glucose' inahitaji virutubisho vingine pia kama vile amino acid na mafuta.

Tovuti ya Cancer.com inaeleza kuwa madai ya kuwa sukari "hulisha" seli za saratani si ya kweli na imekanushwa mara kadhaa na wataalamu mbalimbali.

Inajulikana kuwa seli za saratani hutumia glukosi nyingi kuliko seli za kawaida. Lakini, kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Saratani (National Cancer Institute), hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba kula sukari kunafanya saratani kukua. Vivyo hivyo, si kweli kwamba kuondoa sukari kabisa kwenye mlo wako kutasababisha uvimbe kupungua.

Kuacha kutumia sukari kabisa katika mlo wako ikiwemo zinazopatikana kwenye matunda, mboga na nafaka zisizokobolewa unaweza kusababisha matatizo ya utapiamlo kwani seku zote zinahitaji sukari ili kuzalisha nishati.

Mayo Clinic kupitia tovuti yao wanaeleza kuwa sukari peke yake si chanzo cha saratani, vile vile kutumia sukari haisababishi seli za saratani kukua haraka na wala kutotumia sukari haizifanyi seli hizo kukua taratibu.
Back
Top Bottom