Ningependa maswali ya msingi na mwelekeo, sasa km ulishawahi niuliza nikakwambia unazidi tu kuuliza haya ndi mwasali yanayowakimbiza wanaume. Hata ungekuwa ww ndio nimekupenda na ninazidi kukuuliza mwaswali ya ex wako sijui ungejisikiaje? inakuwa km unanilazimisha nirudi kule niliko toka.
Mfano: ukiambiwa tumetengana hapo wewe ni chance yako kukaza kamba uchukue nafasi kwa kujaza mapungufu ya yule wa kwanza, bora ujikite kuuliza alikuwa na tatizo gani huyo uliyeachana naye na wewe utumie hiyo nafasi kujaza na kumpoza mwenza uliyekutana naye. Mie siwesi kukuuliza kila siku eti kwanini uliachana na boyfriend wako, sana sana ukisha niambia siku moja tu inatosha.
Ila nyie wanawake huwa mnamswali ya kujirudia rudia, itapita miezi, miaka pengine mie niliachana na wife au girlfriend na tuna watoto sasa hapo unategemea kuwa hatutawasiliana kujua hali za watoto wetu. Ndoa ikivunjika watoto huwa hawana hatia yoyote ni matokeo yenu nyie mlioivunja na sio watoto.
sasa ukikuta msg ex wangu kanisalimia mara mioja japo kwa miezi kadhaa" vipi baba watoto hujambo" ww eti unakurupuka na kuanza kuninunia sasa unategemea nini?. Km ni kila siku hapo una haki ya kuniuliza.
jaribu kumwelewa mwenzio na kuwa naye karibu, halafu unajua nyie wasichana ni rahisi sana kuwateka wanaume kwa maneno yenu ya upole, ila mkianza kiherehere cha kuwa na jazba hapo ndio huwa mnaharibu. Ulimi wa mwanamke ni rahisi sana kumteka mwanaume na hata km anafanya upuuzi nje anaweza kuacha just because unempa maneno fulani yakamwingia rohoni. Ila jazba huwa inawaponza sana.