Kuachiwa huru kwa Wendi Mrema

babu kavu

Senior Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
120
Reaction score
128
wataalamu wa sheria naombeni mnifahamishe hii imekaa vipi!?

huyu binti alishirikiana na mganga kumuua mama yake na kuufukia mwili wa mama yake nje ya nyumba yao,alikamatwa na polisi walifika mpaka alipomfukia mama yake na taratibu zingine zilifuata mpaka kupelekwa polisi na kesi kuendelea bahati mbaya sikufuatilia Tena nikisubiri TU hukumu yake[emoji16][emoji16]Sasa nimestuka Jana kuona ameachiwa huru na upande wa mashitaka Hauna haja ya kutaka kuendelea na kesi...
 
Aliyesema alishirikiana na mganga kumuua mama yake ndiyo aliyesema hakuhusika.Kuna tatizo hapo?
nimekuelewa,kwa hiyo Kuna uwezekano wa mtu akafanya kosa lililowazi lakini Kama mshitaki akisema hataki kesi iendelee inakuwa imeisha!??
 
Mkuu katika kesi ngumu na zinazohitaji umakini ni pamoja na kesi za jinai kimsingi ili mtu atiwe hatiani ni lazima upande wa jamuhuri wa prove beyond reasonable doubt pasipo na shaka uhusika wa mtuhumiwa

Inapotokea upande wa mashitaka kushindwa kupata ushahidi basi mahakama inaweza kumwachia mlalamikiwa

Au kupitia Dpp wanaweza wakaweka nore prosque kuwa hawana haja ya kuendelea na shitaka
Inavyoonekana vyombo vyetu vya habari vinakosa weledi kwa kumtangaza mtu au mtuhumiwa kama vile amepatikana na hatia

Tusisahau kutumiwa na jambo lingine na kutiwa hatiani ni jambo lingine
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kama jamhuri ikikosa ushahidi usio na shaka basi kesi hakuna.

Evidence beyond reasonable doubt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…