Soka Ndio Maisha Yangu
Member
- Nov 27, 2024
- 43
- 127
Katika moja ya mambo ya maridhiano baina ya Chadema na Mhe.Rais ilikuwa inahusu wafungwa wa kisiasa, Chadema waliomba mchakato wa kisheria uweze kufanyika ili watu wao waliokuwa magerezani waachiwe.
Mbowe aliliongea suala hili akipinga wale waliokuwa wanadai kuwa maridhiano hayakuwa na tija wala faida yoyote.Kimsingi Lissu ndio alisema maridhiano hayana maana na hayakuwa na faida.
Mbowe alikana maridhiano kutokuwa na faida, alisema yapo mambo walifanikiwa na yapo ambayo hawakufanikiwa.
Moja ni hili la watuhumiwa wao kuachiwa magerezani, kweli waliachiwa wote wakabakia mawili, hata Kinana alipokuwa makamu mwenyekiti wa CCM alitolea ufafanuzi suala hilo, waliobakia walikuwa na kesi za mauaji na zilikuwa zinaendelea mahakamani ikiwemo hii ya Sanga.
Kwahiyo hata Sanga kuachiwa leo na mahakama naweza kutabiri kuwa ni utekelezaji wa yale maridhiano ya kipindi kile.
Hivyo naona kabisa maridhiano ya kisiasa ni muhimu sana kuliko kama anavyodhani Lissu,ambaye ni msomi mzuri asiyekuwa na maarifa.
Kwa sababu hata huko ulaya, nchi zinapigana vita huku zikiendelea kukaa mezani.Huwezi kusema maridhiano hayana maana.