Kuachiwa kwa Sanga ni moja ya maridhiano aliyosema Mbowe, hata kama hatumpendi lakini apewe heshima yake

Hivi ni mimi ambaye naona kuna jambo halipo sawa ? Kama mtu hastahili kuwekwa ndani kwanini awekwe ndani in the first place ? Na kama anastahili / alistahili kuwekwa ndani kwanini aachiwe hata kama ni maridhiano ?

Nadhani badala ya kutatua matatizo yaliyopo tunaongeza matatizo kwa jina la kufanya utatuzi....
 
Ingekuwa maridhiano angetolewa na DPP kama Mbowe. Ila Sanga kashinda kesi ya uonevu iliyofubguliwa na serikali dhalimu ya CCM . Halafu hakuna maridhiano kwenye haki ya mtu. Nashangaa Mbowe abayeshangilia kupata Ruzuku kisa maridhiano.
 
Bila "maridhiano" unaamini angeshinda ?

"...mtu yeyote wa Serikali anaweza kumpigia simu jaji akamwambia huyo usimpe hukumu hiyo, usimpe haki yake"

- Rostam (ulimi ulipoteleza)
Sanga ni Tishio kwa nani?
 
Kwa hiyo mtu akionewa, halafu akashtakiwa halafu akaachiwa. Waliomuonea/dhurumu haki yake wanapongezwa kwa kuachiwa mtuhumiwa?! Hivi ni vituko!
 
Karibu Tena uraiani collegemate...miaka minne ya gerezani sio mchezo kabisaa...
 
Maridhiano huku Soka na wenzie hadi leo hawajulikani walipo? Hayo yote si yametokea baada ya hayo yaliyoitwa maridhiano?

Namuunga mkono Lissu, Mbowe ni simba mzee aliyeishiwa mbinu.
Wote ni wazee
1. FA Mbowe-1961..........umri 63.......baba yake alikuwa ni mwana CCM, kakulia kwenye CCM akajikita kwenye biashara. Aliwahi kutaka kujimilikisha sehemu mojawapo ya eneo la mnazi mmoja, akazungushia uzio wa bati tayari kuanza ujenzi, lakini kuna waziri mmoja machachari (RIP) alitibua hilo.
2. TA Lissu-1967...........umri 57..................ana washabiki kutoka ndani ya CCM, ni mwana CCM ijapokuwa halipii kadi. Asingekuwa mwana CCM asingechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…