Kuachwa kwa Icard, chanzo ni Messi au Lopez?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
》Wanda Nara na Maxi Lopez walianza mahusiano mwaka 2006 walipokutana huko Beunos Aires kama nitakuwa nimeandika vema, Argentina wakati Maxi alipokuwa anaanza kucheza mpira katika timu ya Rosario Central anapotoka Lionel Messi. Wakati huo Nara alikuwa ni mtangazaji wa Tv na pia ni mbunifu wa mavazi hali kadhalika ni Muigizaji wa Tamthilia, wawili hawa walifanikiwa kufunga ndoa mnamo mwaka 2008 huko huko Argentina.

》Kwenye ndoa walibahatika kupata watoto watatu wote wa kiume Valentino, Costantino na Benedicto mapenzi yalikuwa motomoto huku jamaa akichezea Sampdoria na Timu ya Taifa ya Argentina wakat huo ikiongozwa na Diego Maradona. Maisha yalikuwa mazuri sana.

》Ilipofika mwaka 2011 Mauro Icardi akasajiliwa timu ya Vijana akitokea Barcelona na mnamo 2012 akawepo kwenye kikosi cha kwanza cha Sampdoria ambapo alikutana na rafiki yake kwa mujibu wa Maxi ambaye ndo alimpokea vizur alipotoka Barca mpk Sampdoria wakati huo ikifanya vizuri kwa hyo Icardi na Maxi wakawa marafiki wa kutupa wakiwa karibu muda wote hata wakat wa mapumziko huko Balbados, Miami, Ibiza na hata Ciril.
》Ilipofika 2013 Mauro Icardi akasajiliwa Inter Milan lakn bado wakawa marafiki na bata wakila wotw yani Wanda, Maxi pamoja na Icardi.
》Urafiki ukaendelea mpk ilipofika likizo ya 2014 ambapo hawakuitwa national team hivyo ikabidi waende kula bata Miami, Florida huko USA.

》Icardi na Wanda hata siku moja hawakuwahi kuwasiliana hata kwa njia ya simu zaidi ya kusalimiana ana kwa ana basi kila mtu anafata hamsini zake, ilitokea kipindi kimoja wakati Inter wanaenda USA kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa mwaka 2014/2015 sasa wakati Icardi yupo Airport akapokea ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kutoka kwa mwanadada mrembo Nara sms hiyo ilikuwa na ujumbe ufuatao ' Sorry shem naomba uniletee ipad mpya' Icardi akatabasamu kisha akarudisha ujumbe mfupi ' don't worry' .

》Hawakuwasiliana tena mpka aliporejea kuanza msimu mpya wa Ligi aliporejea akampatia zawadi yake ya ipad kisha Nara akamjibu 'Nashukuru sana' sasa hapo ndo mawasiliano yao yakakolea na ikafika kipindi Nara akawa hawezi kulala bila kumtext Icardi yakawa mazoea na wakawa wakifanya hvyo bila Maxi kufahamu chochote kama wawili hawa wanawasiliana, ghafla wakaingia kwenye mahusiano hapo ndipo mshikaj akashtuka kuwa wanadate.
》Nara akamwambia sikuhitaji tena na sasa hvi nipo na Icardi kwa hyo Maxi akawa haamini kilichotokea Perfomance uwanjan ikaapungua ikaonekana kisa ni Icardi amempora demu mshikaji wake wa karibi hyo ndo ikawa story sasa kwamba kikulacho kinguoni mwako, wapo waliomlaumu Icardi lkn pia wapo waliomlaumu Nara. Mapenzi yakapamba moto na ikabidi mwanamke afungue kesi kudai talaka kweli alifanikiwa kupewa talaka mnamo Nov 2014 sasa hapo wakawa wapo huru wanafanya wanachokitaka ikiwa kwenda zile sehem za starehe ambazo walikuwa wakienda wote watatu sasa wakawa wanaenda wawili jambo ambalo likazid kumuumiza sana Maxi Lopez, Kulikuwa na mechi ya Ligi kati ya Inter na Sampdoria wawili hawa walikutana lkn hawakupena mikono na kila mechi zilizowakutanisha wakali hawa ikawa hivyo.

》Lionel Messi mchezaji mwenye ushawish mkubwa sana akasema alichokifanya Icardi sio sawa bali ni kuwadhalilisha wachezaji wengine hivyo timu ya Taifa akawa haitwi kwa shinikizo la Messi, Lionel Messi akaapa kuwa kama Icardi akiitwa Timu ya Taifa basi yeye asijumuishwe kwenye hicho kikosi.

》Mpaka leo hii Icardi tangu mwaka 2013 Icardi amecheza mechi 4 tu hajafunga goli hata moja. Icardi ana rekodi nzuri sana amecheza mechi za Klabu 159 amefunga goli 100, hiyo ni rekodi bora sana lakn hajaitwa timu ya Taifa. Katika msimu uliopita 2017/2018 Icardi kacheza mechi 34 kafunga goli 29 ni Cirro Immobile pekee alimfikia kulinganisha na Higuain aliyefunga goli 16. Katika misimu miwili Icardi kacheza mechi 68 za Ligi kuu amefunga goli 53 rekodi bora kabsa kwa Nahodha huyu wa Inter ambaye alichukua kitambaa kutoka kwa Andrea Ranocchia aliyepokonywa kutokana na kutokuwa na mwendelezo mzuri...
》Icardi alifunga ndoa na mrembo Nara mwaka 2015 na wamejaaliwa watoto 5. Manake Wanda jumla ana watoto 5 ukijumlisha na wale alozaa na Maxi.

> Je Kuna sababu nyingne inayofanya Icardi asiitwe Natinal Team au ni hii hii ya Wanda Nara na Maxi kila mtu hajui nje ya pazia kama ndo hii pengine tusubiri mpaka utawala wa Messi uishe labda atarudishwa kundini..





Icardi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]tusubir 2022 .. ..
 
Hili la kutoitwa kwa icardi ni tokana na sababu nje ya uwezo wa kisoka wa icardi.

Messi kama captain wa timu anaushawishi mkubwa sana katika kikosi cha Argentina,na huenda kuitwa kwa icardi kungewachukiza baadhi na kushusha morale ya timu.
 
huyoooo mfia papuchi "" hafai kuitwa Argentina "" kama ameweza kumfanyia rafiki yake hivyo "" sio ajabu anaweza hata "" kupokeA muamala ili afungishe team " yake " ....apart from talent heshima na nidhamu nikitu muhimu mnoo kwa wachezaji"" ona amesabbisha mpka mwenzie kuweza kushuka kiuwezo "" uwanjani"" kwaajili ya tamaa zake
 
nadhani mauro anajuta kufanya alicho fanya..hana tofauti na benzema..kwa wenzetu nidhamu inahusisha both on and off the pitch
 
Icardi ndio basi tena.. hata hiyo 2022 Hatakuwa na nafasi.. kuanzia umri na uwezo utashuka.
Kutakuwa na vijana wengine muda huo..
Ila Argentina pia inamkosa kipa wao Sergi Romero wa man u.. baada ya kuumia mazoezini.
 
Icardi ndio basi tena.. hata hiyo 2022 Hatakuwa na nafasi.. kuanzia umri na uwezo utashuka.
Kutakuwa na vijana wengine muda huo..
Ila Argentina pia inamkosa kipa wao Sergi Romero wa man u.. baada ya kuumia mazoezini.

Majembe yanaumia,, huu mwaka wana bahati mbaya
 
Suala la uitwaji wa Icardi halihusiani kabisa na suala la Max Lopez. Messi amekua na influence kubwa kwenye Argentina, bila yakuwa rafiki wa messi nafasi yako kwenye kikosi ni ndogo mno. Mascherano mpaka leo bado yupo kikosini.

Kiufupi Icardi ni striker bora kabisa number 9 ndani ya argentina kwa sasa. Higuain hamuwezi kabisa yule dogo. Lakini ndo higuain na Aguero ni marafiki wa messi. Hata Dybla ataishia kwenda kusugua bench tu huku messi na rafiki zake wakiwa uwanjani.
Halafu timu ikishafungwa huharakia kumfukuza kocha, wakati kocha mwenyewe alikua akipangiwa na messi kila kitu. washabadilisha karibu makocha wa 5 ndani ya miaka 8. Kwanini asitimuliwe Messi?
Tevez aliachwa kwa mda mwingi timu ya taifa kwasababu ana bifu na Messi.
 
Icardi ndio basi tena.. hata hiyo 2022 Hatakuwa na nafasi.. kuanzia umri na uwezo utashuka.
Kutakuwa na vijana wengine muda huo..
Ila Argentina pia inamkosa kipa wao Sergi Romero wa man u.. baada ya kuumia mazoezini.
Romero yuko na kaitwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…