Hapa ngoja ningalia kwa mtizamo wa kidunia na kimbigu
Kidunia!22
Kwa mwanaume/ mwanamke maumivu ni yale yale yanayoumiza na kukuacha ukitafakari mengi ingawa baada ya muda wote watasau na huku kila mmoja akiamini umri bado unaruhusu na uwezo wa kumpata mwingine atakayempenda kwa dhati na kuanza maisha mapya pia ndoto zote alizokuwa nazo bado zikaendelea kuwepo pasipo pingamizi la aina yoyote
Kidunia!32
Kwa mwanaume:-
Mwanaume ataumia sana na kuona kama amepoteza muda mwingi na umri unakimbia lakini bado anauweza wa kutafuta mwanamke anayempenda na wa umri wowote kwake na kummiliki pia hata kutimiza ndoto zake zooote alizopanga katika maisha bila vikwazo ,
Kwa mwanamke:-
Ooops Kwa mwanamke ataumia saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana na sana kwa sababu akianza kuhesabu umri umeenda ataanza kukata tamaa kama kweli atakuja kumpata mwenza wa ndoto zake atakayetimiza matarajio yake ,
Mwanamke atanyong'onyea na kuwa mwingi wa mawazo huku akiamini sasa itabidi aanze kucheza pata potea
Na ndio maana wengine hujikuta wamejitumbukiza katika mahusiano yasiyo mazuri na kuanza ku-regret baadae kisa tu anaona umri unaenda na mambo hayaeleweki
Na inatokea wengine wanaamua kuzaa tu huku matumaini yanaendelea kufifia:A S 39:
Upande wa kimungu katika imani zaidi
Miaka 22 /32 (mwanaume na mwanamke)
Kumweka mungu kwanza asimamie maisha yako na kuamini kila jambo linawezekana kwake na kujua kuwa kila jambo huwa linatokea kwa sababu maalum
Itakupa faraja ya kuendelea kuishi kwa amani na huku ukiamini mwenyezi mungu ana makusudi makuu na maisha yako kama amekuumba ni yeye mwenye jukumu la kukutimizia mahitaji yako yote ya kiroho na kimwili
*Kwani alisema niite nami nitakuitikia nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua*
Hivyo basi hutakiwa kukata Tamaa zaidi ni kuomba na kushukuru ukijua moyoni mwako yupo mwenyezi mungu aliyemuweka maalumu kwa ajili yako,Na hasa ukijua duniani kuna mapito na hiyo ni mojawapo ya mapito katika maisha yako haijalishi uko 22,32,42 ,nk nk
Amen