Kuagiza bajaji kutoka nje ya nchi

Kuagiza bajaji kutoka nje ya nchi

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari wana JF.

Naomba kupata Mwanga kwa yeyote ambaye amewahi kuagiza Bajaji (JVC) Mpya toka India (Kiwandani) au kupitia kwa mawakala wao wa kimataifa. Mambo ambayo natamani kuyajua ni haya yafuatayo:-

1. Je unaweza kuuziwa Bajaji moja au lazima ununue idadi kadhaa za Bajaji?

2. Je ukiagiza Bajaji (JVC) kwa moja moja au kwa Jumla (Bajaji kadhaa) bei zinakuwaje?

3. Je Kodi za TRA zinakokotolewa vipi kwa maona katika kikokotoo chao (Tool)hakuna option ya Bajaji?

4. Je kiulinganifu, kununua Bajaji nje ya nchi Moja Moja au Jumala na kununua Bajaji hapa Tanzania kwa wakala wao, ni option ipi ina unafuu?

5. Ningefurahi pia kujua changamoto (Angalizo) katika kuagiza Bajaji JVC toka India au kwa wakawa wao.

Ahsante kwa Ushauri na mwongozo wako
 
4. Je kiulinganifu, kununua Bajaji nje ya nchi Moja Moja au Jumala na kununua Bajaji hapa Tanzania kwa wakala wao, ni option ipi ina unafuu?
Ni rahisi iwapo utanunua mwenyewe hapa nchini kwa wakala wao, kuliko wewe kuagiza.
 
TRA watakuua. Wakikokotoa na kukwambia 20M ukizingatia huku nyumbani ni 7.2M nadhan utajiharishia.
 
Back
Top Bottom