Kuagiza bidhaa Alibaba

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
108
Reaction score
170
Katika kuagiza bidhaa China tuanzie mfano huu wa alibaba.
1-kwanza itabidi ufungue sanduku la posta katika tawi lolote lililo karibu na wewe
2-itabidi upate account ya benki na uwe unamiliki MasterCard au Visa card ya benki yoyote ile au mtandao wa simu yoyote ambao wanatoa huduma ya master card(ila ukipata master card lazima uombe benki wakupe form maalumu ujaze ili uweze kuruhusiwa kufanya manunuzi yako mtandaoni maana bila wao kuruhusu hivyo hutaweza kununua
3-ukishakamilisha hatua hizo mbili hapo juu kinachofuata ni ww sasa kufungua akaunti yako kwenye mtandao husika mf,alibaba ambapo utajaza taarifa zako kuanzia majina yako yote, namba ya simu(ianzie+255),kisha utaingiza nchi,mkoa,wilaya na sanduku lako la posta.

NB: Hapa chini kuwa makini sana zingatia haya
1-wauzaji wote wa alibaba ambao wanatambulika wana nembo kuu tatu.
AπŸ™trade assurance-ina nembo ya dhahabu) hii inakuhakikishia ulinzi wa fedha zako na mzigo wako wakati wote mzigo unapoweka order yako na pia hata ikitokea mzigo umefika halafu mbovu utafidiwa na pia mzigo usipofika kwa wakati maalumu pia utasaidiwa
BπŸ™onsite inspection-nembo ya blue) hii inadhihirisha kuwa muuzaji huyo anajulikana na alibaba kuwa ni muuzaji halisi kama hana nembo hii basi achana nae
CπŸ™experience certification-nembo ya njano) hii inaonesha product zake ziko legit kwa kuuzwa kwenye site ya alibaba muda mrefu.

Kama muuzaji hana nembo hizo 3 hapo juu usinunue utaishia kupoteza pesa zako na pia hata kama muuzaji ni legit kitu cha kwanza unatakiwa kuweka order yako kwa sample ndogo kwanza kisha ukiridhia ubora wake utaweka order kubwa.

NB: Malipo yanafanyika kupitia alibaba tu usije ukalipa nje ya alibaba utalizwa aisee. Nimeweka picha hapo chini ili muone alibaba kunafananaje.

NB: Gharama za usafirishaji inategemea na wewe unataka njia ipi na kila njia ina gharama zake mf express, aircargo, sea freight nk. Mzigo unachukua siku3-30 kulingana na wewe unalipia aina ipi ya usafirishaji.

Kama una swali uliza ila kwa leo/sasa tuishie hapo kwanza
 
(ila ukipata master card lazima uombe benki wakupe form maalumu ujaze ili uweze kuruhusiwa kufanya manunuzi yako mtandaoni maana bila wao kuruhusu hivyo hutaweza kununua
Hii naomba kukupinga, nimenunua vitu kutoka Alibaba kwa kutumia Mastercard ya M-pesa bila kuwa na sanduku la posta Wala kujaza form yoyote bank. Hii saa nilinunua Alibaba

 
Hii naomba kukupinga, nimenunua vitu kutoka Alibaba kwa kutumia Mastercard ya M-pesa
Ukisoma neno kwa neno, point #2 Utabaini
  • Mwenzio anazungumzia Physical Card unayopewa benki
  • Wakati wewe unazungumzia Virtul Card
Kimsing Card zote za benki (Physical Card), kiusalama, by default ZIMEZUIWA kufanya online transaction, Ila ukiwaeleza ndio wanaruhusu.

Hivyo kwa maelezo yake mleta mada yeye yuko sahihi kwa upande wake.

Na wewe Bwana PGO upo sahihi kwa upande wako.

Terms za Virtual card ni tofauti na zile za benki, Je umewahi kusoma Terms za Vodacom MasterCard, au nikuwekee ujisomee na kubaini tofauti?

kufanya miamala mtandaoni: Kuna baadhi ya benki hadi ujaze fomu na kuna benki zingine ukiwaeleza tu wanashughulikia bila kujaza fomu, Hili ni moja.

-----πŸ‘‡
My Take
Tatizo liko kwa mleta mada kwenye #2 hajapangilia vyema, ili kuondoa mkanganyiko.
Japokuwa mimi nimemsoma na kumuelewa.
 
Mpwa Mimi hatasijawahi kuzisoma Wala sijui kama zipo, niliweka pesa nikafanya manunuzi, last month nikaambiwa card ime-expire nikarudishiwa pesa yangu kwa M-pesa
 
Hizo card unatengeza kwa Vodacom tu au hata tigo? Na utaratibu upoje kama inawezekana
 
Safi sana
 
Hii naomba kukupinga, nimenunua vitu kutoka Alibaba kwa kutumia Mastercard ya M-pesa bila kuwa na sanduku la posta Wala kujaza form yoyote bank. Hii saa nilinunua Alibaba

View attachment 2048909
Ilifikajee sasa!? Maana Mimi najua lazima uwe na sanduku la posta ambalo mzigo wako utafikia,,hebu tupe maujanja inawezekana sisi tunazunguka sana aisee
 
Virtual Cards waweza kutengeneza kwa
  • Tigo
  • Airtel
  • Vodacom

Fuata maelekezo kwenye menu ya simu yako kwa mtandao husika/ google search pia ili kuona maelekzo ya maandishi/video
Tr Nielekeze kwa tigo natengenezaje?
Nimewasiliana nao Sipati ushirikiano. Mbn voda na Airtel ni faster sana
 
Kimfano mie nilioder homethieter akajibu wakala Nairobi anadai lipa kwa mpesa mie nikashituka itanifikia kwa masaa6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…