Kuagiza bidhaa China

Kuagiza bidhaa China

MATELLA

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
6
Reaction score
0
habari,naomba kwa ambae amewahi agiza bidhaa za online anipe mwongozo mfano bidhaa ikifika posta au ofisi za DHL kuna gharama gani za kulipa kama kodi??mfano umeagiza simu,nguo n.k
 
nenda kwenye ofis zao ukapate maelezo ya kutosha maana ofis zao zipo karibu mikoa yote
 
ikifika posta kamna wanaotuma wameimark kama GIFT with value less than $10 hamna kodi....ila ukitumia DHL wanalipa kodi wenyewe pale customs then wewe wanakulima kwenye final invoice
 
Kitu cha kwanza na muhimu ni kuwa na hakika na uaminifu wa yule atakayekuuzia mzigo. Maana matapeli ni wengi sana online.

Ukishaelewana naye bei,utamtumia pesa kwa njia mtakayokubaliana. Utamwambia unatumia kampuni gani ya usafirishaji kisha atakupiagia hesabu ya mzigo wako + shipping cost hadi ulipo.

Kama utatumia DHL mzigo ukifika custom wanalipia kodi zote zinazotakiwa kisha wanakuletea hadi ulipo..utawarudishia gharama zao za kodi unapokuwa unapokea mzigo.

My take: Nimekuwa nikitumia DHL muda fulani,ila jamaa wale ni wasumbufu sana wakati mwingine. Kama utaweza kutumia kampuni nyingine ni afadhali..
 
Back
Top Bottom