Kuagiza gari na autocom Japan

Kuagiza gari na autocom Japan

Nimeagiza gari kupitia hawa jamaa autocom japan week mbili sasa sijapata mrejesho kutoka kwao, na hivi hawana office hapa bongo basi nabaki kujifariji tu sijapigwa na kitu kizito mwaka huu lols
Vumilia mkuu kuna mwaka nilinunua kwa SBT gari ikakaa miezi mitatu wakati nimezoea miezi miwili tu Beforward nilianza kupanic lakini ilifika
 
Mkuu habari, ilikuchukua muda gani tangu ufanye malipo mpka gari yako kusafirishwa?
Mimi nimelipia gari week mbili sasa ila wamekua kimya wakisema nisubir ipatikane meli ya kusafirisha
Ni kawaida
 
Gari zao zina ubora, na bei nafuu kulinganisha na soko, unaweza kuagiza, local representatives atakupigia simu, hakikisha pesa unalipa kwenye account ya autocom japan.
Hawa Trust Japane naona they are too cheap to be True.😅🤣
 
Nimeagiza gari kupitia hawa jamaa autocom japan week mbili sasa sijapata mrejesho kutoka kwao, na hivi hawana office hapa bongo basi nabaki kujifariji tu sijapigwa na kitu kizito mwaka huu lols
Autocom nadhani Wana Ofisi bongo aiseee
 
Autocom na Autocj si ni moja??
Kama ndio, basi wana offisi bongo maana nakumbuka miaka kadhaa nyuma niliagizia ofisini kwao kipindi kile ilikuwa kwenye jengo la Quality plaza

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Ni hao hao. Vumilia, wiki 2 si nyingi sana. Mara ya kwanza gari ilisafirishwa haraka tu baada ya kulipia, mara ya pili ilisubiri kama wiki 2 au 3. Inategemea na schedule ya meli.
Pia unaweza kuwasikiana moja kwa moja kwa whatsap na contact person wako akakuambia inasafirishwa lini, na meli gani na lini inategemea kufika
 
Aisee Sijui ni nini hao Trust kwangu mimi naona wana bei za kurusha. Autocom Japan nawakubali nishaagiza kwao zaidi ya mara moja.

Trust ni kweli wana bei kidogo na wana gari chache ila naona kama gari zao zimenyooka sana. (Ni personal experience, sio fact)
 
Trust ni kweli wana bei kidogo na wana gari chache ila naona kama gari zao zimenyooka sana. (Ni personal experience, sio fact)
Nimetembelea website yao naona hawako Wazi sana kama Beforward na Sbt. Car prices hawajumlishi Freight costs. Mpaka uanze kubagain
 
Nimetembelea website yao naona hawako Wazi sana kama Beforward na Sbt. Car prices hawajumlishi Freight costs. Mpaka uanze kubagain

Hujajua tu jinsi ya kunavigate hiyo website yao. Unapata bei ya kila kitu hadi freight na extras. Then ndo unaweza ukaanza negotiation tokea hapo. Haina tofauti sana na website nyingine
IMG_5302.jpg
 
Back
Top Bottom