Kuagiza gari toka japani au kokote nje ya tz

AMAFUMU

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
221
Reaction score
113
jamani naomba kujua ni documents zipi unatakiwa upate na lini zitakufikia ukiwa umeagiza gari nje....naomba msaada kwani kuna meli inaingia 15 aug ina gari yangu toka japan.
 
Aliyekuuzia gari anatakiwa kukutumia doccument inayoitwa Bill of Lading (B/L). Hiyo ndio doccument ya lazima kwa nchi zote.
Lakini kwa vile TRA watataka kujua thamani ya gari, utahitajika kuonyesha risiti ya kununulia hilo gari. Kama huna sio tatizo lakini TRA watafanya makadirio yao yanayoweza kukuumia.

Kama gari linatoka Japan, aliyekuuzia ataambatanisha JAAI au another inspection ya kuthibitisha kuwa gari liko katika hali nzuri ya kiufundi.

Vitu hivyo vitatu pamoja na funguo mojawapo unaweza kutumiwa mara tu gari lako linapoingizwa kwenye meli kwa ajili ya kuanza safari ya Tanzania.

Cha msingi ni kwamba tafuta agent atakayeshughulikia utoaji wa gari lako in advance. Usingoje mpaka gari lifike.

Kama hufahamu kampuni hata moja. Jaribu kucheck na hawa jamaa (I am just giving you one example ili upate kwa kuanzia in case hufahamu any). Hawa wana uyoefu wa magari ya Japan and certainly sehemu nyingine:
DELUXE CARGO SERVICES
Uhuru/Lumumba Road, Workers Development Corp (T) Ltd Building 4th Floor Room No. 2
Dar es Salaam, Tanzania

Email: cargodeluxe@gmail.com
TEL: +255 22 218 1680 / +255 713 767 189
FAX: +255 22 218 1680
 
thanks kaka na nilivyo kuelewa niwasiliane na muagizaji wa gari yangu sio.....but ni lini hasa documents hizo natakiwa niwe nazo je ni pale meli wanapakia au ikiwa imeshafika?

kifupi mi ninadocument moja tu hadi sasa nilipewa ikiwa inapakiwa japani but up to now sijapata nyingine tena ila meli nazani inafika tarehe 15 mwezi huu!
 
Mkuu umechelewa sana kupata docs ungemwambia akutumie soft copy wakati unasubiria hzo B/L! Gari ikishatoka japan ndani ya week inatakiwa uwe ushapata docs fanya fasta mwambie akutumie softcopy uzitoe copy umtafute agent akalog kwenye system ya tra.
 
mkuu hadi sasa nina B/L so nipe ushauri zaidi ili nimpigie simu sasa hivi thanks in advance
 
mkuu hadi sasa nina B/L so nipe ushauri zaidi ili nimpigie simu sasa hivi thanks in advance

Kama una B/L 50% umemaliza, mtafute agent uwe naye perpendicar ili usije pata stored siku hizi hawazingui sana ndani ya siku 3 ushatoa gari.
 
Mkuu umechelewa sana kupata docs ungemwambia akutumie soft copy wakati unasubiria hzo B/L! Gari ikishatoka japan ndani ya week inatakiwa uwe ushapata docs fanya fasta mwambie akutumie softcopy uzitoe copy umtafute agent akalog kwenye system ya tra.

Tra wanakubaki ku log pdf/photocopies?
 
Mkuu hapa umeniacha. Unaposema TRA wanahitaji kujua gari yako umenunua kiasi gani kwani hiyo information inasaidia kujua VAT au ushuru gani? Nnavyoelewa mimi ile Calculator yao si inamaliza kila kitu kwa maana ya duties zote, au?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ile calculator yao wakati mwingine inaweza kukuumiza. Ikiwa hivyo inabidi agent wako abishane nao kwa kuwaonyesha doccs za bei uliyonunulia.

Hiyo bei inatumiwa kuhesabu VAT na Customs duty.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…