Kuahirishwa kwa kesi Mdude ni kielelezo cha kiburi cha Watumishi wa Umma Tanzania

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mahakama inapanga tarehe ya kusoma hukumu ya mtuhumiwa, tarehe inafika na mtuhumiwa anafika mahakamani the mahakama inadai hukumu haijakamilika na mtuhumiwa kurejeshwa rumande kwa zaidi ya siku 14.

Hakimu Kama huyu analipwa pesa na serikali na hakuna sehemu utasikia viongozi wake wakilalamika kuhusu aina hii ya watoa maamuzi. It's like normal to them, Ni Kama wamehukumu tayari na hawaoni Tena nafasi ya mtuhumiwa kuhesabiwa huru Hadi siku ya hukumu.

Najiuliza Hawa mahakimu wapo busy kiasi hicho? Hakimu kwa siku anasikiliza kesi moja au akiamua kwa wiki nzima anaingia mahakamani kuahirisha kesi Kisha anaendelea na majukumu binafsi. Hawa mahakimu wetu wamejengwa kuwa miungu watu, na wananchi tusipowaelekeza kubadilika wataendelea na mtindo huu huu wakukandika hukumu moja kwa mwezi mzima au ziadi.

Lakini pia mahakama upo uwezekano inaingiliwa na kikundi Cha watu wanaopenda wananchi wanyanyasike. Sidhani Kama hukumu hii haipo tayari ila wapo reviwers nje ya judicial wanafanyia kazi.

Lini mahakama mtajiweka huru? Angalieni wenzenu KENYA mjifunze.
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana. Ila hii serikali yetu
 
Sisi ni Mateka wa CCM,Mungu atukomboe kutoka kwenye makucha ya hili jinamizi la Kijani
Hiyo mimba uliyodungwa na mwendazake itakutoa roho kwa siku lazima umtaje mara 62!

Mdude alikamatwa na cocaine za mbowe akizisambaza mikoa ya nyanda za juu kusini
 
Hao itakuwa ni mahakimu mabaki wa yule jamaa ,sasa wanasaboteji tu ili wamtwishe lawama Raisi mpya mwenye harufu ya kuanza kupendeza.
 
Mbona inaonekana kama umekerwa sana na mwenzio kutumia uhuru na haki yake ya kutoa maoni juu ya mahakama in connection na kesi hii ya Mdude Nyangali..??

Katika maelezo yako yooooote haya, hoja yako ni nini hasa hapa...?

Maana mimi binafsi naona unafoka tu na kumrushia maneno yasiyo na staha (matusi) mtoa hoja mwanzo mwisho kiasi cha mtu asomaye kujua moja kwa moja (labda) una mental problem a.k.a kuchanganyikiwa ...!!
 
Asante kwa kumuelimisha! Amenikera mno kwa mtindo wake wa uwasilishaji wa hoja japo sijaiona hoja yake ilipo!
 
Unyanyasaji,kuna watuhumiwa wanatolewa rumande usiku bila Remove Order ila kuna ambao wanapangiwa hukumu mwezi kabla ila mahakimu mwezi unaisha na hukumu bado haijakamilika kuandikwa!Injustice acts from Judicial staffs.
 

Huo sio uhuru. Uhuru kama angejitukana mwenyewe kwa Siri. Lakini ukiair pumba hapa lazima unyoshwe. Tofautisha uhuru na uropokaji. Unapogusa rights za wengine ndo break ya uhuru wako.
 
Hiyo mimba uliyodungwa na mwendazake itakutoa roho kwa siku lazima umtaje mara 62!

Mdude alikamatwa na cocaine za mbowe akizisambaza mikoa ya nyanda za juu kusini
vip wewe uliyetoa mimba ya Mbowe kumbe ndo maana karibu kila posti yako lazima umtaje unahasira naye,mdude anateseka kwa ajili ya kumkosoa mwendazake hakuna lingine
 
Mtoa mada hujitambui. Hujui kuna muda ambao unatakiwa usipite bila hukumu kusomwa? Miezi tatu ndio muda wa mwisho
 
Baadhi ya Mahakama za Tanzania zinatumika kama sehemu ya mateso kwa baadhi ya watuhumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…